Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa
Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love

 

SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato la kiasi cha Sh 4.1 bilioni katika kipindi cha mwaka 2022 hadi kufikia wiki mbili zilizopita. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 8 Februari 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu,Dk.Emmanuel Sweke alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dodoma juu ya Maendeleo ya mamlaka hiyo toka imeanzishwa kisheria mwaka 2010.

Dk.Sweke amesema kuwa licha ya kuwa Uvuvi ni gharama kubwa lakini umeweza kuliingizia Taifa mapato kwa njia za utoaji leseni kwa meli za ndani na nje ambazo zinataka kufanya biashara ya uvuvi katika bahari kuu.

“Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu umekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa meli ambazo zinatakiwa kufanya uvuvi na kuhakikisha zinapokuwa zimepewa leseni zinakuwa na bendera ya Tanzania.

“Pamoja na kuwa na bendera ya Tanzania lazina kuwepo na usimanizi wa kulinda usalama wa wavuvi na meri zao huku kuhakikisha hakuna uvuvi haramu ambao umekuwa ukijitokeza katika bahari hiyo,”ameeleza Dk. Sweke.

Katika hatua nyingine amesema kuwa mamlaka katika kulinda usalama wa bahari kuu wameweka mifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meli ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika.

Dk.Sweke amesema kuwa Mamlaka hiyo inatoa leseni kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya jodari na kueleza kuwa inapotokea mwombaji anafanya tofauti unakamatwa.

Akizungumzia maendeleo ya mapato ndani ya bahari kuu amesema tayari mwekezaji kutoka nchini Uhispania anatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitajengwa katika bandari ya Tanga.

Amesema kuwa mpaka kiwanda hicho kikamilike kitagharimu kiasi cha dola milioni 10,kitazalisha ajira kwa watanzania 100 na kinatarajiwa kuchakata takribani tani 200 kwa siku.

Sambamba na hilo ameeleza kuwa bado mamlaka inakabiliwa na changamoto ya ajira ya moja kwa moja hivyo wapo katika mkakato wa kuanza kutoa ajira kwa maafisa na waangalizi.

Aidha amesema toka Mamlaka kuanzishwa imefanikiwa kukamata meli moja iliyokuwa na tani 100 ya samaki wasiolengwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!