VIJANA wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wameshauriwa kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji ili waweze kujiajiri na kuajiri wezao badala ya kuendelea kuinyooshea vidole Serikali kwa kushindwa kuwapata ajiira. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 8 Septemba 2023 na Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Justen Sangulah alipozungumza kwenye kikao cha baraza la vijana kilichofanyika wilayani humo.
Amesema kuwa badala ya kusubiri serikali itoe ajira kwa upande wao wanatakiwa kujikita kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji ambapo utawawezesha kujiajiri wenyewe na kuajiri vijana wezao.

“Wilaya yetu ya Bahi ina sifa ya kuwepo kwa sekta mbalimbali ambazo zinazoweza kuwabadilisha vijana kimaendeleo na kiuchumi, hivyo niwaomba badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini ni vema wakajikita kwenye fursa hizo ambazo zitawabadilisha maisha yao” amesema.
Sangulah pia amewataka vijana wa Wilaya hiyo kuiunga mkono serikali kwa juhudi zinazofanywa katika kuliletea Taifa maendeleo huku pia wakikataa kutumiwa na watu wasioitakia mema nchi hii kwa lengo la kuharibu amani.
Awali akifungua kikao cha baraza hilo la vijana Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo (CCM) amewataka kuungana kwa pamoja ili kuanzisha vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo itakayowawesha kupata miradi mbalimbali.
Amesema kuwa serikali ipo tayari kuwasimamia kwenye vikundi vitakavyoanzishwa kwa ajili ya kuhakikisha wanapata mikopo ambayo kwa upande wao itawabadilisha mitizamo ya maisha yao.
Leave a comment