Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ushirikiano wa China, Nepal Kutoka kwenye mradi wa BRI mpaka Silk Roadster
Kimataifa

Ushirikiano wa China, Nepal Kutoka kwenye mradi wa BRI mpaka Silk Roadster

Spread the love

MBELE ya vyama kadhaa vya kisiasa na mashirika ya kijamii, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kilizindua jukwaa la “Silk Roadster” wiki iliyopita huko Bhaktapur kama sehemu ya Mpango wa Belt and Road Initiative (BRI) nchini Nepal. Kathmandu Post imeripoti … (endelea).

Nepal iliidhinisha makubaliano ya mfumo wa BRI mwaka wa 2017.

Miaka sita imepita bila kutekelezwa mradi hata mmoja licha ya serikali ya Nepal kuidhinisha makubaliano ya BRI. Huku serikali ikichagua miradi tisa kutekelezwa chini ya mfumo huo.

Maafisa wa China walisema kuwa jukwaa hilo ni wazo jipya lililoletwa Nepal kuadhimisha miaka kumi ya pendekezo la Rais Xi Jinping wa China la BRI.

Silk Roadster ni jukwaa jipya la ushirikiano wa kivitendo na mabadilishano ya watu kati ya China na nchi za Kusini-mashariki na Asia ya Kusini, kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya mpango huo .Kwa kuratibu rasilimali kutoka serikali za mitaa, vyuo vikuu, makampuni ya biashara na taasisi nchini China.

Silk Roadster’ inalenga kufanya mafunzo ya ujuzi wa kiufundi, huduma kwa watu, miradi ya masomo ya nje ya nchi, mabadilishano ya muda mfupi, ushirikiano kati ya makampuni ya biashara na maonyesho ya kitamaduni na kubadilishana matukio na nchi za Kusini-mashariki na Kusini mwa Asia.

Kuna miradi mitano chini ya jukwaa—Ukuzaji wa Barabara ya Hariri, Uwezeshaji wa Barabara ya Hariri, Furaha ya Barabara ya Hariri, Mwangaza wa Barabara ya Hariri na Uboreshaji wa Barabara ya Hariri—ambayo itatekelezwa kupitia vyama mbalimbali vya kisiasa vya Nepali na mashirika ya kijamii.

“Hapo awali, tuliambiwa kuwa BRI ilikuwa inahusu miradi mikubwa inayohusu miundombinu, uunganishaji, bandari, reli, viwanja vya ndege, mitambo ya kuzalisha umeme na mawasiliano, lakini kwa sasa imehusisha miradi midogo ikiwamo ya kutoa mafunzo, ujuzi wa ujenzi, ufadhili wa masomo na mabadilishano ya muda mfupi ya sekta mbalimbali,” kiongozi wa UML aliyehudhuria hafla hiyo aliliambia gazeti la moja na kuomba hifadhi ya jina.

“Hii inaweza kuwa ni kuondoka kwa dhana ya BRI, ambayo sasa imebadilishwa ili kujumuisha miradi midogo hadi midogo. Dhana hii mpya [Silk Roadster] iko katika hatua changa, kwa hivyo hatujui itakuwa na athari gani na itapata majibu na mwitikio gani kutoka kwa vyama vya siasa vya Nepali na serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!