Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Mganga mfawidhi mbaroni madai wizi wa dawa, vifaa tiba
AfyaTangulizi

Mganga mfawidhi mbaroni madai wizi wa dawa, vifaa tiba

Spread the love

Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linamshikilia mtumishi mmoja aitwaye Rioba Nyamos (34) ambaye ni Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji Cha Iporoto akiwa anaiba dawa mbalimbali za  binadamu mali ya Serikali. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 21 Julai 2023, Kaimu Kamanda wa mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi Rashid Ngonyani amesema mbinu aliyotumia ni kuficha katika mifuko ya salfeti Ili dawa hizo zisionekane kisha aende kuziuza maeneo ya Mlowo.

Kaimu Kamanda amebainisha  dawa hizo kuwa ni Ciprofloxacin box 10, belo 3 za vyandarua, Gauzen absorbent 2 PCs, Vidonge vya uzazi wa mpango Boxi 7, Gauze bunda 02 Surgical gloves boxi 10.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda huyo ametoa wito wananchi kutojihusisha na uhalifu kwani Jeshi la Polisi halitosita kuchukua hatua kali dhidi yao.

Pia limewataka watumishi wa Serikali kuacha tamaa kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali pamoja na dawa kwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

error: Content is protected !!