May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ushindi mwembamba wamkera kocha Yanga

Spread the love

CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga hakufurahishwa na namna timu yake ilivyocheza dhidi ya Namungo FC, kwenye mechi ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Licha ya kuibuka na alama tatu kwenye mchezo huo kwa Yanga kuitandika Namungo 1-0 jana tarehe 8 Januari 2021, kocha huyo ambaye ni raia wa Burundi, amesema Yanga haikucheza vizuri.

“Nitabaki na ushindi tulioupata, lakini content (jinsi mchezo ulivyokuwa), haikuwa vizuri hata kidogo, lakini kwa leo (jana) tunakamata hiyo pointi tatu,” amesema Kaze alipozungumza na waandishi kuhusu mchezo huo.

Ameeleza kwamba, miongoni mwa sababu kwa wachezaji wake kuteleza kwenye maeleo aliyokuwa akiwapa, ni changamoto waliyokutana nayo na presha ya mashabiki kwenye mechi hiyo jambo lililochagiza kupatikana kwa ushindi mwembambea.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga

“Naona wachezaji tulionao ni wachezaji vijana, ndio mara ya kwanza wanacheza kwenye timu kama hii yenye presha na washabiki kama hawa, unakuta maelezo ninayompa anakosa jinsi ya kuyakamata,” amesema.

Yanga ina alama tatu katika michezo yake miwili aliyocheza kwenye michuano hiyo, mchezo wa kwanza alitoka suluhu ya bila kufungana na Jamhuri ya visiwani humo.

error: Content is protected !!