Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM ateta na kigogo wa China, aomba msamaha
Habari za Siasa

JPM ateta na kigogo wa China, aomba msamaha

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Ijumaa tarehe 8 Januari 2021, Chato mkoani Geita na kufuatiwa na tukio la Rais Magufuli kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kwa kipande cha kuanzia Mwanza hadi Isaka kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya ujenzi ya China Civil Engineering Construction Company (CCECC).

Kipande hicho ni cha tano katika mradi mzima wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa, ambacho kina urefu wa kilometa 341 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Januari 2024 kwa gharama ya Sh.3.06 trilioni zinazotolewa na Serikali ya Tanzania.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Wang Yi ameipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kujenga barabara na miundombinu mingine kama China ilivyofanya na kwamba hatua hiyo itaisaidia Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kama China.

Akirejea maelekezo yaliyotolewa na Rais wa China, Xi Jinping alipofanya ziara yake ya hapa nchini na ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo, ameziagiza kampuni za China zinazofanya kazi za ujenzi hapa nchi kufanya kazi hizo kwa ubora na kwa maslahi ya Tanzania.

Kwa upande wake, Rais Magufuli ameishukuru China kwa ushirikiano wake na Tanzania katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi na amemhakikishia Wang Yi kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.

Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya CCECC iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa reli kati ya Mwanza na Isaka na ameeleza matumaini yake makubwa kubwa kampuni hiyo itafanya kazi nzuri ya ujenzi.

Amemshukuru Rais Xi Jinping ambaye kwa kumtuma Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje, Wang Yi kuja nchini kuwasilisha ujumbe wake na kwamba nae amemtumia, Rais Xi Jinping ujumbe ukiwa na masuala muhimu matatu ya kuendeleza ushirikiano katika uchumi.

Masuala hayo ni kuomba ufadhili katika miradi miwili ya uzalishaji umeme katika Mto Ruhudji na Mto Lumakali.

Pia, kujenga kilometa 148 za barabara kuu Visiwani Zanzibar na pia, ameomba kupatiwa msamaha wa madeni yakiwemo deni la Dola za Marekani Milioni 15.7 lililotokana na ujenzi wa reli ya Tazara, deni la Dola za Marekani Milioni 137 lililotokana na ujenzi wa nyumba za askari na deni la Dola za Marekani Milioni 15 lililotokana na ujenzi wa kiwanda cha Urafiki – Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesisitiza, Tanzania na China ni ndugu na marafiki wakubwa ndio maana Tanzania imezipatia zabuni kampuni za China katika ujenzi wa miradi mikubwa ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kampuni za China zilizofanya kazi Tanzania zimelipwa zaidi ya Sh.21 trilioni (sawa na zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 10) zilizotokana na kodi za Watanzania.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa China kuja kuwekeza hapa nchini na pia, China kununua mazao ya Tanzania yakiwemo chai, kahawa, pamba na korosho hasa ikizingatiwa kuwa China yenye idadi ya watu takribani Sh.1.6 bilioni ni soko kubwa la bidhaa mbalimbali zikiwemo korosho ambazo wanahitaji zaidi ya tani Sh.700 milioni kwa mwaka.

Rais Magufuli pia amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji wa China kuwa kwa kuwekeza Tanzania watajihakikishia soko kubwa la Afrika Mashariki lenye watu milioni 165 na soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu takribani 500.

Mara baada ya kuwasili hapa Chato hapo jana, Wang Yi alifungua Chuo cha VETA cha Chato na kuchangia Sh.350 milioni kwa ajili ya kununulia vifaa vya uvuvi na leo asubuhi ametembelea na kujionea shughuli za uvuvi katika Mwalo wa Chato ambapo amechangia Sh.45 milioni kwa ajili ya kuboresha Mwalo huo.

Wang Yi ameondoka hapa nchini na kuelekea Ushelisheli ambako anaendelea na ziara yake.

Pamoja na ushirikiano uliopo kwenye sekta nyingine ikiwemo sekta ya miundombinu, uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kuimarika zaidi katika sekta ya Tehama.

Kupitia kampuni ya Huawei, China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya Tehama sambamba na kukuza na kuibua vipaji vya sekta hiyo muhimu hapa nchini.

Matunda ya ushirikiano huo yalijidhihirisha hivi karibuni ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alikabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la Tehama duniani lililoandaliwa na kampuni ya Huawei ambapo wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) walishika nafasi ya pili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!