Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru ‘amshambulia’ Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru ‘amshambulia’ Mbowe

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally
Spread the love

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekinzana na kauli aliyoitoa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba, chama hicho kimeiba kura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Bila kumtaja jina, Dk. Bashiru wakati akikagua jengo jipya la CCM, Chato tarehe 8 Januari 2021 alisema, kauli zilizotolewa na kiongozi huo kuwa, chama hicho kiliiba kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, ni za uongo.

“Nitumie fursa hii kujibu uongo wa kiongozi mmoja wa upinzani aliyekuwa anatoa salamu za Mwaka Mpya kwa kusema uongo,” alisema.

Mbowe kwenye salamu zake za Mwaka Mpya 2021 aliituhumu CCM kwamba, waliiba kura na kuvuruga uchaguzi.

Alikwenda mbali kwa kudai, CCM kwa ilipofika, haiwezi tena kushindana na Chadema hivyo, chama hicho kinatumia mabavu na vyombo vya dola kubaki madarakani.

“CCM hawana uwezo wa kushinda uchaguzi ulio huru na haki katika maeneo mengi ya nchi yetu,” alisema Mbowe.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Kauli ya Mbowe ilitanguliwa na ya James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama NCCR-Mageuzi aliyoitoa katika slaamu zake za Mwaka Mpya 2021.

“Uchaguzi wa mwaka uliopita umeliacha Taifa uchi na kuliaibisha. Mtu anayeachwa uchi anapaswa kujisitiri dhidi ya aibu pindi tu anapogundua yuko uchi,” ameandika kwenye waraka huo,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Uchaguzi wa mwaka 2020 ulikuwa uchaguzi usiozingatia matakwa ya ukuaji wa demokrasia na ustawi wake.

“Uchaguzi huo ulijaa ubinafsi na kunufaisha watu wachache katika taifa letu, tofauti kabisa na matarajio ya ustawi wa demokrasia ya nchi ili kukuza maendeleo yetu na maslai ya watu wengi.”

Hata hivyo, Dk. Bashiru amewataka CCM kutonyamazia uzushi huo na kwamba, haukibaliki kwa kuwa una nia ovu kwa nchi.

“Uzushi huu wenye nia ovu kwa nchi yetu haukubaliki na wanaCCM msikae kimya kwenye uzushi kama huu,” alisema Dk. Bashiru na kuongeza:

“…muungwana ni mtu ambaye vitendo vyake na kauli zake vina manufaa kwa jamii yake na taifa kwa ujumla,” alisema.

Aliwaeleza wana CCM hao kwamba, mafanikio ya chama hicho yalitokana na mambo manne ambayo ni kuwepo mikakati ya chama kujitegemea, kujenga chama kuwa kiungo na daraja kati wananchi na serikali yao, kuongeza wanachama na kusimamia maadili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!