BALOZI wa Marekani katika Umoja wa Mataifa , amesema kuwa mataifa ya Afrika hayawezi kubaki kutounga mkono upande wowote katika vita ya Ukraine. Inaripoti BBC.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Linda Thomas – Greenfield kuzungumza na BBC na kubaini kuwa katika kura ,iliyopigwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu, wiki mbili zilizopita zilionesha kuchukiwa kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine katika ,nchi 17 za Afrika, ambazo ni nusu ya Dunia nzima , zilijizuia na nyingine nane hazikupiga kura kabisa.
Hata hivyo Balozi huyo alisema kwamba hakuweza kuwa na msingi kwenye kutoegemea upande wowote , kwakuwa mgogoro huo haukuwa wa mashindano ya Vita Baridi kati ya nchi za Magharibi na Urusi .
Aidha Thomas -Greenfield amesema, Marekani ilikuwa ikisaidia kutafuta vyanzo mbadala vya bidhaa ambazo nchi huagiza kutoka Urusi.
Mwanadiplomasia huyo amesema kwamba Marekani itaunga mkono pendekezo la Afrika Kusini la Kupatanisha Urusi na Ukraine.
Leave a comment