NCHINI Burundi Mkulima mdogo wa zao la Mahindi ametoa mchango wa kilo 100 za mahindi kwa wale waliokimbia ghasia nchi Ukraine.
Kijana huyo ambaye zamani alikuwa mkimbizi anayefahamika kwa jina la Adrien Nimpagaritse alikuwa yatima akiwa na umri wa miaka minne alipokimbilia nchini Tanzania, wakati wa wimbi la ghasia za kikabila mwaka 1996.
Alisema alilelewa katika kambi ya wakimbizi ya Mutenderi , ambako alisoma shule na kurejea nyumbani Burundi baada ya miaka 11 mwaka 2007 , akiwa na umri wa miaka 15 .
‘’Niliona jinsi wakimbizi wanavyokuwa wakiishi hatukuweza kupata chakula ‘’ alisema.
‘’Iwapo mtu , Jirani angekupa jani la muhogo tu au maji ungeshukuru sana ‘’
Hata hivyo Nimpagaritse sasa anaishi katika jimbo la Ruyingi mashariki mwa Burundi , ambako ameoa na kufanikiwa kupata Watoto watatu.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alimtaka mtu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , kuja kuchukua mchango wake wa mahindi kwa ajili ya Ukraine .
Pia amesema yeye ana sauti ya kuchangia katika kuleta suluhu la mzozo huo, lakini anaweza kuchangia baadhi ya kile alichokilima kama ishara ya upendo.
Aidha amehimiza kama kuna mtu yeyote, aliye na moyo kama huo wa kusaidia tunaweza , kuwasaidia karibu familia 20.
‘’Binafsi ninaweza kumudu kutoa kilo 100 za mahidi , haitoshi ,kwa hivyo ikiwa kuna mtu mwingine ataongezea zaidi itasaidia’’
Leave a comment