Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Umahiri wa Kingereza wanafunzi Tusiime wamshangaza Ofisa Elimu Dar 
Elimu

Umahiri wa Kingereza wanafunzi Tusiime wamshangaza Ofisa Elimu Dar 

Spread the love

 

UMAHIRI wa hali ya juu wa kumudu kuzungumza lugha ya kingereza kwa ufasaha ulioonyeshwa na wanafunzi wa shule ya msingi Tusiime umemfurahisha Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid na kuwaduwaza wazazi waliohudhuri mahafali yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Maulid alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 19 ya shule hiyo ambayo yamefanyika leo shuleni hapo Tabata jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi kuonyesha umahiri wao kwenye maigizo mbalimbali kwa lugha ya kingereza.

Mbali na mgeni rasmi wazazi nao walionekekana kupigwa na butwaa kutokana na namna wanafunzi hao wa shule ya msingi walivyoweza kumudu kuzungumza lugha ya kingereza kana kwamba wako vyuo vikuu.

Igizo lililowakuna wengi akiwemo mgeni rasmi na wazazi wa wanafunzi hao ni lile ambalo mmoja wa  wanafunzi wanaohitimu kuigiza kusoma taarifa ya habari kwa lugha ya kingereza bila kutetereka.

Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid akimpa cheti mmoja wa wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu darasa la saba kwenye shule ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam kwenye mahafali yaliyofanyika leo shuleni hapo. Anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule, Jonson Kapira na Mkurugenzi wa shule za Tusiime, Dk. Albert Katagira

Kwenye taarifa hiyo ya habari Mwanafunzi mwingine wa darasa la tano alionyesha uwezo mkubwa wa kufanya uchambuzi hali ambayo iliwafanya wazazi wengi kubaki na mshangao.

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Maulid aliwapongeza walimu wa shule hiyo na Mkurugenzi wa shule hizo, Dk. Albert Katagira kwa namna walivyoweza kuwaandaa wanafunzi hao kitaaluma na wengine kuzungumza kingereza kama wamezaliwa nacho.

“Nimewasikiliza wanafunzi wanavyozungumza kingereza kwenye masuala mbalimbali kwa kweli wazazi mtaungana namini kusema kwamba hamkukosea kuleta watoto wenu hapa Tusiime, binafsi nimeshangazwa na umahiri wa wanafunzi hawa huwezi kuamini kwamba wako shule ya msingi,” alisema Maulid na kuongeza

Wanafunzi wa shule ya msingi Tusiime wakiigiza igizo la Sinderera wakati wa mahafali ya 19 shuleni hapo
4. Wanafunzi wa shule ya msingi Tusiime ya Tabata Dar es Salaam wakijiandaa kutumbuiza kwa igizo maalum wakati wa mahafali ya 19 yaliyofanyika shuleni hapo

“Kwenye taaluma mmekuwa mkifanya vizuri mwaka hadi mwaka na leo nimeona kitu kingine hapa. Lugha ya kingereza imenyooka si mchezo kwa kweli walimu mnajitahidi sana endeleeni na moyo huo,” alisema Maulid

Mmoja wa wazazi aliyekuwa kwenye mahafali hayo, Antony Nazael alisema siku ya leo ameshuhudia mambo ambayo yamemshangaza kwani hakutarajia mwanafunzi wa shule ya msingi anaweza kuwa mahiri kwa kiwango alichoona

“Mwanafunzi aliyesoma taarifa ya habari kwa lugha ya kingereza mtu anayesikiliza anaweza kudhani kwamba ni taarifa ya habari kweli kutokana na lugha nzuri ya kingereza na mpangilio mzuri kumbe ni maigizo tu. Nawapongeza walimu wamefanyakazi kubwa sana kuwapika,” alisema

Wanafunzi wa shule ya msingi Tusiime ya Tabata Dar es Salaam wakijiandaa kutumbuiza kwa igizo maalum wakati wa mahafali ya 19 yaliyofanyika shuleni hapo

Mzazi mwingine, Kassim Jumbe alisema mwanafunzi aliyefanya uchambuzi wa masuala mbalimbali ya michezo yanayoendelea nchini ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kingereza ameifanya siku yake kwenda vizuri kwani ameonyesha kipaji cha aina yake.

“Yule mwanafunzi atakuwa mchambuzi mahiri sana wa michezo siku za usoni nimemsikiliza vizuri amenofurahisha sana na hivi ndivyo vipaji ambavyo tunapaswa kuvilea na kuviendeleza kama alivyosema mgeni rasmi,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!