WATU 29 wamefariki na wengine 16 wamepotea kutokana na mafuriko yaliyotokea katika jimbo la Hebei nchini China. Imeripotiwa na Global Times … (endelea).
Mamlaka ya jimbo la Hebei imewaambia waandishi wa habari jana Ijumaa tarehe 11 Agosti 2023 kuwa imetenga kiasi cha Yuan 95.811 bilioni kwa ajili ya kujihami na maafa hayo.
Mamlaka hiyo imethibitisha vifo hivyo pamoja na kutoa rambirambi kwa familia zilizofiwa pamoja na kuwafariji wathirika wa mafuriko hayo.
Naibu Gavana wa Jimbo wa hilo Zheng Chengzhong amesema kuwa mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na kimbunga.
Wizara ya Fedha pamoja na ile ya dharura nchini humo imeongeza pesa nyingine kiasi cha Yuan 1.46 bilioni kwa ajili ya kudhibiti maafa hayo.
Mpaka sasa serikali ishatumia kiasi cha Yuan 7.738 bilioni kwa ajili ya uokoaji katika majimbo matano ambayo ni Beijing, Tianjin, Hebei, Jilin na Heilongjiang.
Serikali ya China imetuma timu ya uokoaji katika maeneo yaliyoathiriwa kwa ajili ya kuwaokoa wananchi na imesema kuwa mpaka kufikia tarehe 1 Septemba wanafunzi wote watakuwa washarejea shuleni huku wananchi waliopoteza makazi wakipatiwa makazi mapya.
Watu 1.75 milioni wamehamishwa kwenye makazi yaliyoathiriwa ambapo tayari Serikali ishakarabati barabara 2237 zilizoharibika.
Leave a comment