Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Ulega: Kaya milioni 2.2 zinajihusisha na ufugaji
BiasharaHabari Mchanganyiko

Ulega: Kaya milioni 2.2 zinajihusisha na ufugaji

Spread the love

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kaya milioni 2.2 nchini Tanzania zinajihusisha na sekta hiyo na kuchangia ukuaji wa uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ulega amesema hayo leo Jumatano wakati akiwasilisha taarifa yake katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula (AGRF), linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Amesema sekta ya mifugo ina mchango mkubwa mkubwa katika shughuli za kiuchumi ambapo kaya milioni 2.2 nchini Tanzania (asilimia 35) zinajihusisha kwenye eneo hilo 

“Katika kipindi cha mwaka 2023 sekta imewezesha tani 805,000 za nyama, lita bilioni 3.6 za maziwa, mayai bilioni 5.5, na ngozi tani milioni 14.1 kupatikana,” amesema

Alisema  matumizi nyama kwa mtu mmoja ni kilo 15, maziwa lita 62 na mayai 106 kwa mwaka ikilinganishwa na viwango vinavyopendekezwa vya kilo 50, lita 200, na mayai 300.

Waziri Ulega amesema mauzo ya nje ya sekta ya mifugo yameongezeka ambapo tani 14,700 za nyama, kilo 65,000 za maziwa, na vipande 800,000 vya ngozi vimeuzwa na kuchangia ya dola za Marekani milioni 63.

Ulega amesema sekta ya maifugo ina vyanzo mbalimbali vinavyofaa kwa uwekezaji, ikiwemo idadi kubwa ya mifugo ambayo ni takriban milioni 77. 

“Mazingira ya agro-ekolojia mbalimbali yanayosaidia uzalishaji wa aina tofauti za wanyama wa mifugo, kama vile eneo la Kusini linalofaa kwa uzalishaji wa maziwa, Kati na Ziwa yanayofaa kwa uzalishaji wa ng’ombe na mbuzi, na Kaskazini linalofaa kwa nyama ya ng’ombe na kondoo,”amesema.

Amesema pia upatikanaji wa ardhi inayoweza kusaidia uzalishaji wa malisho na uzalishaji wa mbegu za malisho ni fursa nyingine.

Waziri huyo amesema soko la wanyama wa mifugo na bidhaa za wanyama wa maifugo lipo kwa wingi nchini Tanzania yenye zaidi ya watu ya milioni 61.

“Pia kuna soko la Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Kusini kwa Jangwa la Sahara (SADC), na Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) lenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.4,” amesema.

Aidha, amesema katika kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya mifugo, wameondoa baadhi ya kodi, ada, na vikwazo visivyo vya ushuru katika biashara ya mifugo na bidhaa zake.

Ulega amesema kuongezeka kwa huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na huduma za bima ambazo zimeongezwa kwa tasnia ya wanyama wa mifugo, pia ni fursa nyingine.

“Kubwa kuliko ni utulivu wa kisiasa nchini Tanzania na rasilimali watu ikiwa ni pamoja na vijana na wanawake,” amesema.

Amesema kutokana na fursa hizo wizara ina mikakati wa utekelezaji wa Mpango wa Kubadilisha Sekta ya Mifugo (LSTP) ambao unajumuisha maeneo saba muhimu.

Ulega amesema pia wanaboresha ng’ombe bora wa kuzaliana kwa kuwapatia malisho na maji safi.

“Kuongeza nguvu katika mfumo wa afya ya wanyama kupitia kampeni za chanjo na udhibiti wa magonjwa,” amesisitiza.

Waziri Ulega amesema bidhaa za mifugo zinachangia katika kuboresha ubora wa lishe na afya nzuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!