Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Profesa UDSM ataka shule ziige ubunifu kwa shule za St Mary’s
Elimu

Profesa UDSM ataka shule ziige ubunifu kwa shule za St Mary’s

Spread the love

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Goodluck Urassa amesema ili shule ziweze kufanya vizuri kitaaluma, walimu wanapaswa kufanya kazi yao kama sehemu ya biashara, na kuongeza ubunifu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Profesa Urassa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwajengea uwezo walimu wa shule za Kimataifa za St Mary’s, ili waweze kuongeza ubunifu na ufanisi katika ufanyaji kazi wao.

Alisema lengo la semina hiyo ni kuwapiga msasa walimu hao, katika mambo mengi ikiwamo elimu ya ujasiriamali, ubunifu, na namna ya kuongeza ufaulu katika shule zao kwaajili ya kuzikuza kitaifa.

“Nimewapiga msasa namna ya kufanya kazi kwa viwango vya juu, jinsi ya kuhudumia wateja, kuendesha shule zao kibiashara na kijasiriamali” alisema Profesa Urassa

MHADHIRI wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Goodluck Urassa akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwajengea uwezo walimu wa shule za Kimataifa za St Mary’s, ili waweze kuongeza ubunifu na ufanisi katika ufanyaji kazi wao

Pia, aliwataka walimu kujenga utamaduni wa kuwa na mpango, wa kufanya kazi kuanzia mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka, pamoja na ule wa kila siku kwenye kutimiza majukumu yao ya kitaaluma.

“Shule nyingi, zinaathirika kwa kutojenga vizuri mipango yao, na kukosa rasilimiari za kujiendesha ndiyo maana tunawajengea walimu na viongozi uwezo ili wakawarithishe na wanafunzi wao ili tuje kupata viongozi bora wa baadaye” alisema

Vilevile, alizisihi taasisi za elimu kukumbuka umuhimu wa kutoa semina kwa watumishi wa serikali, ili waweze kukumbuka majukumu yao, muhimu wa kazi yao na kuongeza ufanisi katika kazi akisema kuwa njia hiyo itasaidia kupata matokeo chanya kwenye sekta.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Goodluck Urassa akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwajengea uwezo walimu wa shule za Kimataifa za St Mary’s, ili waweze kuongeza ubunifu na ufanisi katika ufanyaji kazi wao.

Mkurugenzi wa shule hizo Tanzania, Dk Rose Rwakatale, alisema lengo la semina hiyo ilikuwa kuwainua wafanyakazi wao, na kuwaongeza elimu ili waweze kutimiza majukumu yao kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Alisema semina hiyo iliwakutanisha walimu kutoka shule 14 zilizopo Dar es Salaam na mikoa mingine kwa lengo la kusikiliza, kuchambua kwa kina na hatimaye kwenda kufanyia kazi Ili kuongeza ufanisi kwenye shule zao.

Mkuu shule ya St Mary’S Tabata, Thomas Samsoni alisifu semina hiyo akisema imewafungua kwa kiasi kikubwa kwani wamefundishwa namna ya kuwahudumia wateja, majukumu ya viongozi katika taasisi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Goodluck Urassa akizungumza jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwajengea uwezo walimu wa shule za Kimataifa za St Mary’s, ili waweze kuongeza ubunifu na ufanisi katika ufanyaji kazi wao

“Baada ya semina hii matokeo yatakuwa makubwa, tumefundishwa vitu vingi, tumeongeza maarifa na ujuzi, imekuwa siku nzuri kwetu kujifunza kutoka kwa Profesa mbobezi tunategemea kuhamishia maarifa haya kwenye maeneo yetu ya kazi” alisema.

Aliushukuru uongozi wa shule hizo kwa kuandaa semina hiyo, aliyoita elimishi akiomba liwe jambo endelevu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!