Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Ufaransa yaonywa kutoingilia kijeshi Niger
Kimataifa

Ufaransa yaonywa kutoingilia kijeshi Niger

Spread the love

Uongozi mpya wa kijeshi nchini Niger umeituhumu Ufaransa kutaka kuingilia kati kijeshi ili kumrejesha madarakani Rais aliyeng’olewa Mohammed Bazoum. Anaripoti Mariam Mudhihiri kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Hayo yanajiri wakati mivutano ikiongezeka kati ya Niger na Ufaransa, iliyokuwa mtawala wa kikoloni kwa Niger, na majirani zake.

Aidha, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Catherine Colonna amekanusha madai hayo jana  Jumatatu jioni na kuongeza kuwa bado upo uwezekano wa kumrejesha madarakani Bazoum.

Kutokana na madai hayo, Serikali za Mali na Burkina Faso zinazoongozwa na wanajeshi nazo zilionya kwamba uingiliaji kati wowote wa kijeshi nchini Niger utachukuliwa pia kama tangazo la vita kwa nchi zao zote mbili.

Bazoum ambaye ni mshirika wa karibu wa nchi za magharibi ambaye kuchaguliwa kwake miaka miwili iliyopita kuliashiria kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu uhuru wa Niger, aliondolewa madarakani tarehe 26 Julai na kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa rais.

Mkuu huyo wa kikosi cha ulinzi wa rais, Jenerali Abdourahamane Tiani alijitangaza kuwa kiongozi, lakini madai yake yalilaaniwa kimataifa na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS) ambayo ilimpa wiki moja kurudisha madaraka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!