Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Baraza la vyama vya siasa laitisha mkutano wa dharura kujadili hali ya siasa nchini
Habari za Siasa

Baraza la vyama vya siasa laitisha mkutano wa dharura kujadili hali ya siasa nchini

Jaji Francis Mungi, Msajili wa Vyama vya Siasa
Spread the love

BARAZA la Vyama vya Siasa nchini, limeitisha mkutano wa dharura kwa ajili ya kujadili hali ya siasa nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

 

Mkutano huo unafanyika leo tarehe 1 Agosti 2023, jijini Dar es Salaam, ambalo viongozi wa vyama vya siasa, dini na wadau wengine wameshiriki.

 

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Juma Ali Khatib amesema wameitisha mkutano huo kutokana na hali ya siasa ilivyo nchini.

“Madhumuni ya kuja hapa kujadili mambo muhimu kitaifa kutokana na hali ya siasa ilivyo sasa ndani ya Taifa letu. Tuliona kina umuhimu tujadili tuangalie namna gani nzuri tutaweza songa mbele tukiwa wamoja,” amesema Khatib.

Naye Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amewataka washiriki wa mkutano huo kutoka na maazimio yatakayosaidia nchi kusonga mbele.

“Tumekuja hapa kujadili kama Watanzania, nimelazimika kusema haya kwa sababu najua watu huko nje wanasubiri kwa hamu kuona huu mkutano utaisha kweli? Wanaenda kutokana macho, hapana. Baraza limeitisha mkutano Maalum kupanua mawazo na kuchangia ili kusonga mbele,” amesema Jaji Mutungi.

Miongoni mwa mada zinazokadiliwa katika mkutano huu, ni pamoja na vyama vya siasa kutumia viongozi wa dini katika shughuli za siasa, mavazi yanayovakiwa na vitendo vya walinzi wa viongozi na Mali za Vyama vya siasa.

Nyingine ni kugha zinazotumika katika mikutano ya hadhara ya vyama hivyo na shughuli nyingine za kisiasa.

Akizungumzia mada hizo, Jaji Mutungi amewataka washiriki wasinyoosheane vidole pamoja na kutuhumiana, bali wajadili namna ya kuleta siasa zenye ushindani nchini.

“Tuondoke hofu tumekuja hapa sio kurumbana kujua vyama vingapi vinatumia viongozi wa dini kufanya siasa, tumekuja hapa kuelimushana namna ya kuendesha siasa zetu kistaarabu,” amesema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi amesema dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ni kuona demokrasia ya vyama vingi zinaijmarika sambamba na kudumusha amani nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!