Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Dodoma, Askofu wacharuka wanaokejeli miradi ya Serikali
Habari za Siasa

RC Dodoma, Askofu wacharuka wanaokejeli miradi ya Serikali

Bwawa la Umeme Rufiji
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka Watanzania kutoibeza na kuikwamisha miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa  kushirikiana na baadhi ya washirika wa kimaendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Amesema hayo juzi Jumapili kwenye Ibada ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la Karmel Assembless of God Tanzania(KAGT) linaloongozwa na  Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Evance Chande.

Ibada hiyo ilikuwa na lengo la kuombea Taifa, Rais, Baraza la Mawaziri na viongozi mbalimbali sambamba na uzinduzi wa kitabu kujulikanacho kama  “ijue nguvu iliyopo katika sifa na kuabudu”.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali, inagharimu mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo ili kukamilika kwa wakati, hivyo  inabidi kila mmoja kuona uthamani wake na kupata ari ya kuilinda ili isihujumiwe badala ya kuinyooshea vidole na kuibeza.

“Kuna baadhi ya watanzania ambao hawaitakii mema na mafanikio yanayofanywa na serikali katika uwekezaji uliopo kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi. Kazi yao ni kulaumu na kuinyoshea vidole hata kama miradi hiyo ina faida kwao.

Naye Askofu mkuu wa Kanisa la Karmeli Assemblies of God Tanzania, Dk. Evance Chande amekemea baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakikejeli miradi hiyo kwa kuikosoa serikali kama haina faida.

Amesema watanzania wana kila sababu ya kumpongeza na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji ambao unaofanyika nchini kwa maendeleo ya nchi.

Alisema miradi yote ipo kwa ajili ya watanzania wote bila kujali itikadi yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!