Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Dodoma: Nane nane iwe na tija kwa wakulima, wafugaji
Habari Mchanganyiko

RC Dodoma: Nane nane iwe na tija kwa wakulima, wafugaji

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema maonesho ya wakulima ya nane nane yanatakiwa kulenga zaidi kutoa elimu kwa wakulima ili kilimo kiwe chenye tija badala ya kuwa ya kujikimu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Aidha, ameeleza kuwa katika kuelekea sherehe za maadhimisho ya Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini ambayo hufanyika kila mwaka nchini kuanzia tarehe 1 Agosti na kufikia kilele tarehe 8 Agosti, kwa Kanda ya Kati imejipanga kuja na mbinu za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 31 Julai 2023, Senyamule amesema utafiti unaonesha mikoa wa Dodoma na Singida imeendelea kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema hali hiyo imeathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo mifugo na uvuvi, hivyo uongozi wa mikoa hiyo umedhamiria kusambaza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira.

Ametaja mbinu hizo kuwa ni pamoja kuhifadhi maji na udongo mashambani ikijumuisha matumizi ya makingamaji, kilimo cha mbegu tisa na jembe la mzambia, kuzalisha mazao yanayotumia maji kwa ufanisi kama vile mtama na alizeti).

Pia uzalishaji wa malisho kwa ajili ya mifugo, uhifadhi ya misitu na upandaji wa miti, matumizi ya nishati mbadala (Jua, umeme na gesi) kwa ajili ya kupikia.

“Tutajikita zaidi kusambaza teknolojia za kisasa katika kilimo na ufugaji bora ambapo taasisi za utafiti za kilimo, mifugo na uvuvi zitashiriki maonesho hayo kuonesha teknolojia mbalimbali zilizozalishwa kwenye vituo vya utafiti na kuwawezesha wakulima kunufaika na elimu ya uzalishaji bora,” amesema Senyamule.

Aidha, amesema katika maonesho hayo kutakuwa na matukio muhimu ikiwemo kongamano la tasnia ya alizeti, mtama, siku maalumu ya uhamasishaji uzalishaji kuku wa kienyeji pamoja na tamasha la mashindano ya nyama choma.

Amesema kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu kitaifa ni “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula” wakati kikanda ni “Kilimo ni Biashara, Biashara ni Uwekezaji.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa...

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

error: Content is protected !!