WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza meneja wa Wakala wa barabara mkoa wa Dar es Salaam kufika katika barabara ya Gomvu – Kimbiji hadi Pembamnazi ili kuona hatua za kuchukua kutokana na ubovu wa barabara hiyo ulitokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Pia amemuagiza mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga barabara ya Kibada – Mwasonga yenye urefu wa kilomita 41 kuendelea kukusanya vifaa vya ujenzi wa barabara hiyo wakati serikali ikijipanga kumpatia malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa barabara hiyo.
Bashungwa amebainisha hayo leo Jumatatu bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile (CCM) aliyehoji lini barabara ya Gomvu – Kimbiji – Pembamnazi itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akijibu swali hilo, Bashungwa amesema barabara ya Gomvu – Kimbiji – Pembamnazi ni sehemu ya barabara ya Mjimwema – Kimbiji – Pembamnazi yenye urefu wa kilometa 49 ambayo inajengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami kulingana na upatikanaji wa fedha.
Amesema kwa sehemu ya Cheka – Avic (km 2) tayari ujenzi umekamilika wakati kwa sehemu ya Avic – Kimbiji (km 10) taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi zinaendelea.
“Aidha, ujenzi kwa sehemu iliyobaki ya Kimbiji hadi Pembamnazi itajengwa kulingana na upatikanaji wa fedha,” amesema.
Tunawatakia kazi njema