Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko AMEND warejea kuwanoa madereva bodaboda
Habari Mchanganyiko

AMEND warejea kuwanoa madereva bodaboda

Waendesha pikipiki (Bodaboda) wakiwa maeneo ya mjini katika shughuli zao za kawaida
Spread the love

Shirika la Amend Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi linatarajiwa tena kuanza kutoa mafunzo ya elimu ya usalama barabara ni kwa madereva wa bodaboda katika kata mbalimbali za jiji la Dodoma ili kuunga mkono jitihada za serikali kudhibiti janga la ajali nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Awamu ya pili ya mafunzo hayo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri kuomba mafunzo hayo yatolewe tena kwa kata zilizosalia.

Katika mafunzo ya awali ambayo yalitolewa Februari mwaka huu, jumla ya madereva bodaboda 250 waliopatiwa mafunzo hayo.

Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend, Amiri Matimba amewaambia waandishi wa habari kwamba mafunzo hayo yataanza kutolewa leo tarehe 15 Aprili 2024 katika kata ambazo hazikupata mafunzo hayo yalipotolewa Februari mwaka huu.

Amefafanua mafunzo hayo yananalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki, abiria na watumiaji wengine wa barabara, hivyo kuzuia vifo na majeruhi wa matukio ya ajali ambapo wengi wao ni vijana.

Ameongeza kuwa Amend na Ubalozi wa Uswisi wamekubali ombi la mkuu wa wilaya ya Dodoma na kwamba mafunzo yanaanza rasmi leo Jumatatu na wadau mbalimbali watashiriki likiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Walimu wa Usalama Barabarani, Mwalimu Massava Ponera amewataka maofisa usafirishaji (bodaboda)kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli zao.

“Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yana umuhimu makubwa kwani mbali na vifo ajali za barabarani husababisha ulemavu wa kudumu huku takwimu za sensa nchini zikionesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na wengi wameamua kujikita katika ujasiriamali wa bodaboda.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!