Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya yaanza kutiririsha matokeo ya Urais
Kimataifa

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya yaanza kutiririsha matokeo ya Urais

Wafula Chebukati, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC)
Spread the love

 

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) hatimaye ilianza kutiririsha matokeo ya urais yaliyothibitishwa mwishoni mwa siku Alhamisi kwa ajili ya kutangaza matokeo ya mwisho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uchaguzi huu umekuwa tofauti na nyakati zilizopita kwasababu Tume ya IEBC, haijatangaza matokeo moja kwa moja kadiri wanavoyapokea.

Hatua hii imeonekana kama njia ya kujaribu kwendana na uamuzi wa Mahakama ya Juu Zaidi wa mwaka 2017, ikiwa ni pamoja na kutojumlisha papo hapo kura zote na kutoa matokea moja kwa moja kwa umma, badala yake jukumu hilo limeachwa mikononi mwa vyombo vya Habari.

Pia kuna hatua zingine zilizofanyiwa maboresho kama vile kifungu cha 138 (3)(c) cha katiba.

Kinachofanyika, Tume hiyo inatumia fomu za 34A zenye matokeo ya urais kutoka kwenye vituo vya kupiga kura 46,229 kote nchini humo.

Ilivyokuwa wakati wa miaka ya nyuma ni kwamba fomu 34A zilikuwa ndio matokeo ya mwisho na tume hiyo haikuwa na nguvu ya chochote baada ya hapo.

Aidha, fomu 34A zilizoidhinishwa zinapatikana kwenye tovuti ya Tume ya IEBC na hapo wananchi wanaweza kujijumlishia wenyewe matokeo yao.

Hatua hii huenda ikasababisha wasiwasi miongoni mwa wananchi wanaofuatilia kwa karibu kujua viongozi wao wajao hasa kutokana na mwendo wa pole wa zoezi hilo kwa jumla lakini mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, amesihi wananchi kutokuwa na hofu na matokeo tofauti yanayotolewa na vyombo vya Habari.

Hata hivyo, Bwana Chebukati ameonyesha kuwa maafisa wa Tume ya IEBC wenye jukumu la kuwasilisha fomu 34A, wanatarajiwa kuanza kuziwasilisha ana kwa ana kuanzia hii leo asubuhi.

“Tunaendesha uchaguzi huu kwa kufuata sheria. Maafisa husika wa IEBC watakapowasilisha fomu 34A na 34B, tutaanza mchakato wa uthibitishaji na kuwapa taarifa Wakenya kuhusu kile kinachoendelea,” alisema katika moja ya mikutano yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!