Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TMA yatoa tahadhari ya mvua ya Masika
Habari Mchanganyiko

TMA yatoa tahadhari ya mvua ya Masika

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a
Spread the love

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua za wastani hadi juu ya wastani kwa msimu wa Masika, 2024 zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msimu wa mvua za Masika ni mahususi kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwan, Dar es Salaam, Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 22 Februari, 2024, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a, amesema mvua hizo zinatarajia kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024 katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi.

Dk. Chang’a ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, amesema mvua hizo za masika zinatarajiwa kuwa na ongezeko kubwa katika kipindi cha mwezi Machi, 2024.

“Kutokana na kuwa na matarajio ya uwepo wa mvua hizo kubwa kutakuwa na vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo,” amesema Dk. Chang’a.

Dk. Chang’a alisema athari nyingine zinazotarajiwa kuongezeka kwa kina cha maji katika mito na mabwawa, magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji.

Kwa upande wa vyombo vya habari, Dk. Chang’a alishauri kupata, kufuatilia na kusambaza taarifa za utabiri na tahadhari, pindi tu zinapotoka ili jamii iweze kuzipata kwa wakati.

“Tunawashauri kutafuta ushauri wa kitaalamu kutoka katika sekta husika wakati wa kuandaa, kutayarisha na kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji. Pia, inapendekezwa kutumia lugha nyepesi wakati wa kuhabarisha jamii,” amesema Dk. Chang’a.

Dk. Chang’a alisema TMA inawashauri watumiaji wote wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na wakulima, wafugaji, mamlaka za wanyamapori, wasafirishaji, mamlaka za maji, afya, shughuli za ujenzi (Makandarasi), uchimbaji madini, upakuaji na ushushaji mizigo bandarini kuendelea kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika.

Pia amesema TMA itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua na hali ya hewa kwa ujumla nchini kadri inavyohitajika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!