Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Tetemeko la ardhi lauwa watu 118 China
Kimataifa

Tetemeko la ardhi lauwa watu 118 China

Spread the love

TETEMEKO la ardhi lililotokea nchini China maeneo ya Kaskazini-Magharibi, limesababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na kujeruhi 397. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, tetemeko hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, likiwa na ukubwa wakipimo cha 5.9, lilipiga katika mikoa ya Gansu na Qinghai, nchini humo ambapo mbali ya kupoteza maisha ya watu, lilibomoa makazi.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa China, Xi Jinping, ameagiza mamlaka za uokoaji zikatoe misaada katika maeneo yaliyoathirika.

Vyombo vya habari nchini China, vimeripoti kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka hadi kufikia 118, wakati juhudi za kuwaokoa waathirika zikiendelea.

Watu takribani 20 hawajulikani na walipo, wakati 2,200 wakiokolewa huku maelfu wakikimbia makazi yao kwenda sehemu zilizo salama.

Wizara ya fedha ya China, imetenga Dola za Marekani 27.9 milioni, kwa ajili ya kushughulikia tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!