Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo TECNO yagusa hisia: Mchezo wa hisani wachochea hamasa ya kuboresha viwanja vya jamii Afrika
Michezo

TECNO yagusa hisia: Mchezo wa hisani wachochea hamasa ya kuboresha viwanja vya jamii Afrika

Spread the love

 

KAMA mdhamini rasmi wa Kombe la  (AFCON) Afrika nchini Côte d’Ivoire, kampuni ya teknolojia , TECNO iliandaa mechi ya hisani iliyojaa nyota magwiji wa mpira wa miguu Africa siku ya pili ya sherehe ya ufunguzi. Mechi hiyo ilishirikisha Katibu Mkuu wa CAF, Véron Mosengo-Omba, wachezaji maarufu wa mpira akiwemo Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf, Asamoah Gyan, Dennis Oliech, na Erick Otieno, waliyoonyesha ushirikiano wao kwa michezo na maendeleo ya jamii.

Meneja Mkuu wa TECNO Akishikana Mkono na magwiji wa Soka Afrika

Picha ya pamoja Timu ya CAF Pamoja na magwiji wa Soka Africa

Kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki, TECNO ilitangaza mpango wa kufadhili matengenezo ya viwanja 100 vya mpira vya jamii zote Afrika ndani ya miaka mitano ijayo. Mpango huu unalenga kuhamasisha ushiriki wa vijana, kukuza maisha yenye afya, na kuhakikisha upatikanaji wa viwanja bora vya michezo katika jamii zisizopewa kipaumbele. Meneja Mkuu wa TECNO, Jack Guo, alisema kwa hamasa, “Tumeanzisha safari ya kuzitia mwangaza ndoto zisizohesabika kwa kuboresha viwanja 100 kote Afrika,” akisisitiza nguvu ya kubadilisha ya mpango wa TECNO. Taylan Tankpinou, mvulana wa miaka 10, aliongeza, “Asante kwa TECNO, tunajenga maeneo bora ya kuchezea na kukua!

Hotuba ya Mpango wa Kifadhili

Ili kuhamasisha zaidi, TECNO ilitangaza kwamba kwa kila goli lililofungwa katika mchezo huo liligharimu, dola $10,000 ambazo zingechangiwa kwenye kampeni hiyo. Mchezo ulimalizika na TECNO kuchangia dola $50,000 zaidi kwa mradi huo. Ahadi hii ilifanya kila goli kuwa shangwe si tu kwa wachezaji bali pia kwa vizazi vijavyo ambavyo vitafaidika na miundombinu bora.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!