Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mama (53) atolewa ganda la pipi kwenye pafu, aliishi nalo miaka 11
Habari Mchanganyiko

Mama (53) atolewa ganda la pipi kwenye pafu, aliishi nalo miaka 11

Spread the love

Watalaam wa Magonjwa ya Mfumo wa Mapafu na Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, leo Jumatatu wamemtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 Akizungumza baada ya kutoa ganda hilo, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dk. Hedwiga Swai amesema mgonjwa huyo alikuja akiwa na tatizo la mapafu yake kuharibika na kutoa usaha vilevile alikua anatoa makohozi yenya harufu kali.

“Mgonjwa huyo alikuja kwa lengo la kufanya vipimo vya kifua (Bronchoscopy) ila baada ya kuingiza kifaa chenye kamera kwenye mapafu tuliona kuna kitu ambacho sio cha kawaida katika pafu lake la kushoto na tulipoangalia vizuri tuligundua kuwa huo haukua uvimbe bali ni ganda la plastiki” amesema Dk. Swai.

Dk. Swai ameeleza kuwa mgonjwa huyo alikua anamng’unya pipi na ganda lake mwaka 2013 kwa bahati mbaya akameza na ganda lake na alipoenda hospitali hawakuona tatizo lolote na baada ya muda alianza kukohoa na kutoa usaha, ndipo alipoanza kutumia dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu bila mafanikio yoyote.

Dk. Swai ameitaka jamii kuacha tabia ya kuchezea vitu mdomoni ambavyo vinaweza kuleta madhara kwakuwa kitu hicho kikingia kwenye mfumo wa hewa kinaweza kusababisha madhara mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!