Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzia; Mbunge CCM afariki dunia
Habari za SiasaTangulizi

Tanzia; Mbunge CCM afariki dunia

Spread the love

MBUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mussa Hassan Mussa Silima wa Jimbo la Amani Zanzibar (CCM) amefariki dunia leo tarehe 13 Oktoba, 2022 nyumbani kwake Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson imeeleza kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Mussa Hassan Mussa. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa jimbo la Amani. Mwenyezi mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,: amesema Spika Tulia.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, mwili wa marehemu unapelekwa kijijini kwao Bwejuu kwa ajili ya maziko yanatarajiwa kufanyika saa kumi leo baada ya sala ya alasiri.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!