Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tendega adai hakupewa nafasi ya kujitetea Chadema
Habari za Siasa

Tendega adai hakupewa nafasi ya kujitetea Chadema

Spread the love

MBUNGE Viti Maalum, Grace Tendega, amedai hakuomba msamaha mbele ya Baraza Kuu la Chadema, dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kukiuka katiba ya Chama hicho kwa kula njama ya kujipeleka bungeni, kwa kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Tendega ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, tarehe 13 Oktoba 2022, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, katika usikilizwaji wa kesi aliyoifungua yeye na wabunge wenzake viti maalum 18, kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Ni kwenye Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, akiulizwa maswali ya ufafanuzi na wakili wake, Ipilinga Panya, dhidi ya maswali ya dodoso aliyoulizwa Ijumaa iliyopita na Wakili wa Chadema, Peter Kibatala.

Wakili Panya alimhoji Tendega anaiambia nini mahakama hiyo kuhusu swali alililoulizwa na Wakili Kibatala, kama alipewa nafasi ya kujitetea katika kikao cha Baraza Kuu la Chadema lililofanyika mwaka huu na kutupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa Chadema.

Na kama alipewa fursa ya kuhakiki rufaa zao na kupokea uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema, wa kumvua uanachama yeye na wenzake 18, kwa tuhuma za kukiuka Katiba ya chama hicho Kwa kujipeleka bungeni bila kuteuliwa na chama.

Ndipo Tendega alijbu akidai kwa mujibu wa aya ya 27 ya hati yake ya kiapo alionyesha kitu ambacho walipewa ni fursa ya kuomba msamaha.

Pia, Tendega alihoji  mtu anaombaje msamaha wakati hajapata haki ya kusikilizwa.

“Katika aya hiyo ya 27 kama nilionyesha kitu ambacho tulipewa ni fursa nilizopata kuomba msamaha. Lakini Jaji unaomba msamaha kwa kipi wakati hukupata haki ya kusikilizwa,” amedai Tendega.

Katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika Mei 2022 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimuuliza kama Tendega na wenzake wana la kusema mbele ya wajumbe, mara tatu, lakini hawakujibu.

Awali, Tendega alidai kuwa, hakupata haki ya kujitetea kwa kuwa alichelewa kupata barua ya wito wa kujieleza na kudai ilitumwa tarehe 26 Novemba 2020, kupitia mtandao wa Whatsapp, lakini kutokana na changamoto mbalimbali aliipokea mchana wa tarehe 27 Novemba 2020, siku ambayo kikao kilikuwa kimefanyika asubuhi take.

Amedai kuwa, baada ya kuchelewa kushiriki kikao hicho, Kamati Kuu ya Chadema ilitoa uamuzi wa kumfukuza uanachama bila ya kumsikiliza na kumtaka akate rufaa au aombe upya uanachama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!