Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Kikula aainisha mikakati tume ya madini uboreshaji sekta ya madini
Habari Mchanganyiko

Prof. Kikula aainisha mikakati tume ya madini uboreshaji sekta ya madini

Spread the love

MWENYEKITI wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha kila mwananchi na kuinua sekta nyingine za kiuchumi na uchumi kuendelea kukua kwa kasi.

Profesa Kikula ameyasema hayo leo tarehe 13 Oktoba, 2022 jijini Mwanza kwenye kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi kilichoshirikisha Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Nsubisi Mwasandende.

Pia Mwakilishi wa Kamishna wa Kazi – Ofisi ya Waziri Mkuu, Goodluck Luginga, watendaji kutoka Tume ya Madini Makao Makuu na kutoka Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa walishiriki kikao hicho chenye lengo la kujadili na kutatua changamoto katika utendaji kazi  wa Tume ya  Madini.

Amesema mikakati iliyowekwa ni pamoja na ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini kupewa kipaumbele ambapo kwa sasa wananchi wameanza kutoa huduma kwenye migodi ya madini iliyoanzishwa nchini na kujipatia kipato, uboreshaji wa miundombinu na huduma nyingine za jamii ili kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kupata kipato ambacho ni endelevu hata mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji wa madini.

Ameongeza kuwa mikakati mingine iliyowekwa sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ni pamoja na kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa na mchango wa asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula amesema Tume ya Madini itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wake kwenye utendaji kazi na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi na kukidhi matarajio ya wananchi hususan wachimbaji, wachenjuaji na wafanyabiashara wa madini.

Awali akieleza mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Tume, Profesa Kikula ameeleza kuwa ni pamoja na kuimarika kwa ukusanyaji wa maduhuli kutoka Sh bilioni 346.78 kwa kipindi cha mwaka 2018-2019 hadi kufikia Sh bilioni 624.61 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021-2022 ikiwa ni sawa na asilimia 96.09 ya lengo la mwaka husika.

Profesa Kikula ameendelea kueleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 83 na ongezeko la utoaji wa leseni za madini ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021-2022 Tume ilitoa jumla ya leseni za madini 9,498 ikilinganishwa na leseni 6,314 zilizotolewa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020-2021.

Aidha, Profesa Kikula amesema ili kusogeza huduma karibu zaidi na wadau wa madini, Tume ilianzisha ofisi mpya za madini katika mikoa ya Mbogwe na Mahenge.

Ameendelea mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umeendelea kukua kutoka asilimia 4.8 katika kipindi cha mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 7.2 katika kipindi cha mwaka 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!