Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yajipanga kuwa kitovu cha tiba Afrika
Habari Mchanganyiko

Tanzania yajipanga kuwa kitovu cha tiba Afrika

Spread the love

SERIKALI  imejipanga kuifanya nchi kuwa kitovu cha tiba utalii, kwa kuweka mikakati itakayosaidia utoaji huduma za afya kwa wagonjwa maalum wa ndani na nje ya Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamelezwa leo tarehe 28 Novemba 2023 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akifungua mradi wa kliniki mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa, iliyopo kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), itakayotoa huduma za kliniki kwa wagonjwa wa ndani na nje ya Tanzania.

“Haya tutakayoyashuhudia leo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa ambao Rais Samia Suluhu Hassan amefanya katika Sekta ya Afya lakini pia niwapongeze Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) chini ya Prof. Abel Makubi na Mwenyekiti wa Bodi Prof. Charles Mkony kwa kazi nzuri na kubwa ya kuokoa maisha ya Watanzania,” Amesema Ummy.

Waziri Ummy amewaomba Watanzania wenye uhitaji wa tiba kwa haraka waende MOI ambapo ndani ya masaa mawili unamaliza kila kitu na kuendelea na shughuli zako.

Aidha, Waziri Ummy ameitaka MOI iendeshe kliniki hiyo mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa kwa ubia na wawekezaji wengine ili kuboresha zaidi huduma zitolewazo.

“Ni jambo zuri sana mmelianzisha lakini tusije kukwama njiani hivyo tushirikiane na wadau wengine ili huduma hii iendelee na ni matarajio yangu kwamba kliniki hii mpya ya wagonjwa maalumu na wagonjwa wa Kimataifa itakuwa kliniki ya mfano ambayo itakua kivutio kikubwa kwa wagonjwa kutoka katika Mataifa mbalimbali,” amesema Ummy.

Amesema, Kutokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu vifaa tiba na wataalamu, Taasisi ya MOl imefanikiwa kupunguza rufaa za wagonjuwa kwenda nje ya nchi ambapo hivi sasa 99% ya huduma za mifupa zinapatikana hapa nchini na 97% ya huduma za kibingwa za ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zinapatikana hapa chini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!