WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Prof. Adolf Mkenda amevitaka vyuo vikuu barani Afrika, kujikita katika kufanya tafiti zitakazojibu changamoto za wananchi, pamoja na kuandaa wahitimu watakaokidhi matakwa ya soko la ajira. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 28 Novemba 2023, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua kongamano la 14 la Wadhibiti Ubora wa Elimu ya Juu barani Afrika (AfriQAN).
“Chuo kikuu kazi yake sio tu kurithisha uelewa, lakini kuzalisha uelewa mpya kwa kufanya tafiti. Vyuo vijikite katika masuala ya utafiti hii itasaidia kupata majawbau ya matatizo ya jamii. Mfano tumekuwa na tatizo la Malarria Ulaya hakuna Malaria , tufanye utafiti kujua kwa nini wenzetu wameweza,” amesema Prof. Mkenda.
Katika hatua nyingine, Prof. Mkenda amezitaka taasisi za elimu ya juu, kuongeza udahili wa wanafunzi, huku akitoa angalizo kwamba ongezeko hilo liende sambamba na ubora wa elimu itakayotolewa.
Leave a comment