Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yachaguliwa kuiwakilisha Afrika Baraza la Utalii duniani
Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa kuiwakilisha Afrika Baraza la Utalii duniani

Spread the love

Tanzania imechaguliwa kuziwakilisha nchi za Afrika katika Baraza Tendaji la Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia 2023 hadi 2027. Anaripoti Regina  Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania ilichaguliwa katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 19 Oktoba 2023, nchini Uzbekistan ambapo ilipita bila kupingwa na nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa UNWTO.

“Tanzania imethibitishwa na Mkutano Mkuu wa 25 wa UNWTO, kuwa mjumbe wa baraza tendaji la shirika hilo kwa kuchaguliwa bila kupingwa na nchi wanachama wa Shirika la UNWTO. Uchaguzi huo umefanyika tarehe 19 Oktoba, 2023 Jijini Samarkand, Uzbekistan ambako mkutano mkuu wa 25 wa UNWTO unaendelea,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Afrika kupitia Tanzania itawakilishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki katika mikutano muhimu ya baraza hilo inayofanyika mara mbili kwa mwaka.

“Akizungumza baada ya Tanzania kuthibitishwa katika nafasi hiyo, Kairuki ameeleza kuwa nafasi hiyo ni muhimu katika kukuza na kutangaza utalii wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuwa Baraza hilo ni chombo muhimu kinacho simamia Mipango na Bajeti ya Shirika pamoja na utekelezaji wake,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Aidha, Waziri Kairuki ameongeza kuwa, kupitia nafasi hii, Tanzania itashiriki kupeleka agenda muhimu zenye maslahi mapana ya maendeleo ya utalii wa Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!