Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania, Czech kuimarisha utalii, biashara na uwekezaji
Habari za Siasa

Tanzania, Czech kuimarisha utalii, biashara na uwekezaji

Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Czech zimekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano hususan utalii, biashara na uwekezaji ili kukuza na kuimarisha misingi ya diplomasia iliyopo baina ya mataifa hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, amebainisha hayo alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Martin Tlapa leo tarehe 3 Oktoba, 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema kuwa Tanzania ilisaini mkataba wa ushirikiano na Jamhuri ya Czech mwaka 2006 hivyo sasa ni wakati muafaka wa kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano.

 

“Ni muda tangu tuliposaini mkataba wa makubaliano hivyo kwa sasa ni wakati muafaka baina yetu Tanzania na Czech kuingia mkataba wa makubaliano katika maeneo mapya ya ushirikiano hususan katika sekta biashara na uwekezaji, Utalii,” amesema Balozi Mbarouk

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa katika sekta ya utalii, miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa inapokea watalii 6,000 kutoka Jamhuri ya Czech, na kwa kuwa maambuzi ya uviko 19 yamepungua duniani, Tanzania imeboresha mazingira ya utalii na sekta nyingine kama vile biashara na uwekezaji, hivyo nawasihi watalii na wawekezaji kutoka Czech kuja kutalii na kuwekeza Tanzania.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Martin Tlapa amesema kuwa Czech inajivunia ushirikiano wake imara na wa muda mrefu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuahidi kuwa Czech itaendelea kudumisha ushirikiano huo.

“Naukuahidi kuwa tutaendelea kuwahamasisha watalii, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Czech kuja kutalii na kuwekeza Tanzania…..ni jukumu yetu kuhakikisha kuwa sekta ya biashara na uwekezaji inakuwa na kunufaisha mataifa yote mawili,” amesema Tlapa

Tlapa amesema Czech itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano kama vile elimu, afya, kilimo, utamaduni na michezo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Tlapa yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 2 – 4, Oktoba 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!