Monday , 13 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Tax awasili wizarani
Habari za Siasa

Dk. Tax awasili wizarani

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax amewasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dkt. Tax aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Oktoba 2022 na kuapishwa tarehe 03 Oktoba 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Dk. Tax amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula baada ya Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri.

Mara baada ya kuwasili Katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Dk. Tax amesema atafanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wote wa Wizara katika kila ngazi ili kuhakikisha kuwa malengo ya Wizara yanatekelezeka.

“Nipo tayari kufanya kazi na nyinyi, na kujifunza kutoka kwenu ili kuniweze kutekeleza majukumu yangu… taasisi yoyote ili iweze kufanikiwa lazima kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano,” amesema Dkt. Tax

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wizara kutumia Sh. 3.5 bilioni kuchunguza afya ya akili, nguvu za kiume

Spread the loveWIZARA ya Afya, imepanga kutumia Sh. 3.50 bilioni, kwa ajili...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC yapaza sauti changamoto ya intaneti

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umeitaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Prof. Ndakidemi aitaka TMA kutoa taarifa kwa njia ya SMS

Spread the loveMBUNGE wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) ameishauri Serikali...

error: Content is protected !!