Friday , 24 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele
AfyaHabari za Siasa

Wizara afya kutumia Sh. 1.31 trilioni, huduma za kibingwa zapewa kipaumbele

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

WIZARA ya Afya, imeliomba Bunge lipitishe makadirio yake ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, ya kiasi cha Sh. 1.31 trilioni, huku ikitaja vipaumbele 10 vilivyopangwa kutekelezwa katika bajeti hiyo ijayo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Bajeti hiyo imeombwa leo tarehe 13 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Miongoni mwa vipaumbele vilivyotajwa na Ummy ni uimarishaji huduma za kinga dhidi ya magonjwa ambapo kiasi cha Sh. 117.61 bilioni. Sh. 219.01 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya afya katika ngazi zote.

“Kipaumbele kingine ni kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini, ambapo kiasi cha 6.00 bilioni kimetengwa kutekeleza afua zake,” amesema Ummy.

Huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto zimetengewa Sh. 17.18 bilioni, wakati kiasi cha Sh. 74.00 bilioni zikitengwa kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji watalaamu wa sekta ya afya katika fani za kati,ubingwa na ubingwa bobezi.

Kipaumbele kingine ni kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi nchini, ambapo imetengwa Sh. 89.85 bilioni kwa ajili ya utekelezaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo

Spread the loveRAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 63 ya Uhuru bila katiba ya wananchi

Spread the loveWAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanaharakati...

AfyaMakala & Uchambuzi

Uongo, uzushi, tiba ya matende, ngiri maji

Spread the loveKUNA uongo na uzushi katika jamii kuhusu wanaume, wanawake na...

error: Content is protected !!