Thursday , 9 May 2024
Home Kitengo Biashara STANBIC, AGRICOM kuanza kutoa mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima
Biashara

STANBIC, AGRICOM kuanza kutoa mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima

Spread the love

BENKI ya Stanbic Tanzania (SBT), kwa kushirikiana na kampuni ya AgriCom Africa (AA), inatarajia kuanzia kutoa mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima ili kuleta Mapinduzi katika sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Hati ya makubaliano ya awali kuhusu suala hilo, imesainiwa Jana Jumapili, Katika Viwanja vya Nanenane, jijini Mbeya.

Mkuu wa Kitengo Cha Mikopo ya Asseti na Vyombo vya Moto, kutoka SBT, John Mosha, amesema hatua hiyo inalenga kuleta Mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza matumizi ya zana Bora na za Kisasa katika kukuza sekta hiyo nchini.

Mosha Amesema ushirikiano huo itasaidia wananchi kunufaika na zana mbalimbali za kilimo zilizotengenezaa kwa telnolojia Bora na ya Kisasa kutoka Kampuni ya AA.

Mbali na mikopo ya zana, Mosha amesema kupitia huo wananchi wataweza nufaika na mikopo ya fedha katika sekta ya kilimo biashara kwa zaidi ya asilimia 80 kutoka Benki ya Stanbic ambapo wataweza kulipa ndani ya miezi 60 (miaka mitano).

“Ushirikiano huu utahakikisha upatikanaji wa zana za Kisasa ambazo ni bora, wakulima watanufauka na zana hizo zitakazoweza kusaidia kuongeza uzalishaji kwenye shughuli za shamba hivyo kuhamasisha maendeleo ya kilimo biashara,” amesema Mosha.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka SBT, Fredrick Max,  amesema mpango huo umejikuta Katika kukuza mnyororo wa thamani kwenye kilimo biashara kwa kubuni mifumo inayoongeza uzalishaji, uchakataji na usafirishaji mahitaji Katika kilimo.

“Pamoja na mambo mengine, SBT tumejikita Katika kulea vijana na wanawake wajasiriamali waliopo Katika kilimo biashara kupitia programu ya biashara atamizi. Programu hii inalenga kuhamasisha vijana kuingia Katika kilimo,” amesema Max.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AA, Alex Duffar, amesema makubaliano hayo yanalenga kuchagiza matumizi ya zana za kilimo  Bora na Kisasa.

“AgriCom tumejidhatutu kuhamasisha matumizi ya zana za kilimo kupitia ushirikiano kama huu ambayo Leo tumeuingia na Stanbic Bank Tanzania,” amesema Duffar.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amesema makubaliano hayo yataongeza thamani sekta ya kilimo.

“Kilimo cha sasa ili ufanikiwe unahitaji mashine za Kisasa, hivyo makubaliano haya yatawezeaha zana za kilimo kwa wakulima na kurahisisha kilimo hatimaye kusaidia azma ya Serikali ya kwamba ifikalo 2030 Tanzania iongeze uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa asilimia 10,” amesema Homera.

Mpango huo wa ushirikiano umetajwa kuwa na lengo la kuunga mkono ajenda ya 10/30 ambayo inalenga kukuza sekta ya kilimo kwa zaidi ya asilimia 10 ifikapo 2030, pamoja na kuhakikisha usalama wa upatikanaji chakula nchini na kuongeza mapato kutoka Dola za Marekani 1.2 bilioni Hadi Dola 5 bilioni ifikapo 2030.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Moon of Thoth, historia ya Misri ya kale ilipofichwa ndani ya kasino

Spread the love  Nchi ya Misri imebeba karibia asilimia kubwa ya mambo...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

Biashara

Expanse Tournament kasino mzigo umeongezwa hadi mil 400/=

Spread the love Jiunge na Meridianbet kasino kufurahia promosheni kubwaya Expanse Tournament,...

Biashara

Bounty Hunters sloti yenye utajiri Meridianbet kasino

Spread the love Congo DR inasifika sana kwa wingi wa madini ya...

error: Content is protected !!