Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yaahirisha hukumu ya kesi ya ‘DP Word’
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yaahirisha hukumu ya kesi ya ‘DP Word’

Spread the love

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Mbeya, leo Jumatatu, imeahirisha kutoa uamuzi wa shauri la madai lililofunguliwa na raia watano, wanaopinga makubaliano ya kibiashara na uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam, nayohusisha serikali ya Tanzania na Dubai. Anaripoti Mwandishi Wetu…endelea.

Usomaji wa hukumu hiyo umeahirishwa kufuatia taarifa kuwa mwenyekiti wa jopo la majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, kupata hudhuru.

Shauri lililofunguliwa na raia hao wane, linapinga makubaliano ya uwekezaji kati ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kampuni ya DP World ya Dubai, yafutiliwe mbali.

Kesi ya kupinga makubaliano ya uwekezaji ilifunguliwa ikiwa na hoja sita, ikiwamo kutaka ufafanuzi wa tafsiri na baadhi ya vipengele vilivyoko katika makubaliano.

Kesi hiyo namba 05/2023 inawahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge.

Pamoja na kufunguliwa kwa shauri hilo, mjadala mkubwa umekuwa ukiendelea nchini Tanzania, tangu kuibuka kwa suala hilo, kisha Bunge la taifa kuridhia Juni 10 mwaka huu.

Mkataba wa uwekezaji uliobua mjadala, malumbano na hata kurushiana maneno, ulisainiwa 22 Oktoba mwaka jana.

Baadhi ya wanaokosoa makubaliano hayo, akiwamo mwanawazuoni mahiri wa sheria nchini, Prof. Issa Shivji, wamedai kuwa mkataba umelalia upande mmoja.

Kwamba, mkataba mzima unatoa haki kwa Dubai na kuifanya Tanzania kuwa na wajibu wa kutekeleza.

Prof. Shivji, anaungwa mkono na Prof. Anna Tibaijuka, anayetaka kuwapo kwa mjadala wa kitaifa.

Prof. Tibaijuka, kabla na baada ya Bunge kuridhia mkataba huo, amesimama kukosoa na kutaka mkataba usitishwe, hadi kutolewa elimu kwa jamii ili kulinda maslahi ya taifa.

Hatua hiyo, imesababisha kuzuka kwa pande mbili; upande unaounga mkono mpango mzima wa uwekezaji wa bandari na ule unaopinga baadhi ya vipengele vilivyomo ndani ya mkataba na kutaka vipengele hivyo virekebishwe kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mkataba baina ya serikali na mikataba mingine mahsusi ya uwekezaji inayotarajiwa kuigiwa hapo baadaye.

Bandari za Tanzania, hususan bandari ya Dar es Salaam ni suala muhimu la kiuchumi kutokana na kutegemewa kimapato kwa huduma zake za ndani ya Tanzania nan chi nyingine majirani zaidi ya tano zisizokuwa na bandari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!