Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko THRDC yalia ukata wasaidizi wa kisheria, yataka wafike gerezani
Habari Mchanganyiko

THRDC yalia ukata wasaidizi wa kisheria, yataka wafike gerezani

Spread the love

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imesema kuna uhaba wa watu wanaotoa msaada wa kisheria, kitendo kinachopelekea wananchi kukosa haki ya kufikia vyombo vya kisheria ili kupata haki zao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, jijini Dar es Salaam, katika semina ya siku mbili (tarehe 7 hadi 8, Agosti 2023) kuwajengea uwezo watoa huduma ya msaada wa kisheria 60, kutoka mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema Tanzania Ina wasaidizi wa kisheria 5,000 ambao hawatoshi kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 60, hususan wa maeneo ya vijijini.

Mbali na uhitaji mkubwa wa wasaidizi hao katika maeneo ya vijijini, Olengurumwa amesema Kuna haja kubwa ya watoa huduma za msaada wa kisheria kuwepo katika magereza yote nchini

“Tumezunguka huko tumeona Kuna haja ya magereza kuwa na watoa msaada wa kisheria, pia tunataka maeneo yote ambayo msaada wa kisheria unahitajika Watanzania wasiikosw huduma hiyo. Watanzania tuko zaidi ya milioni 60, ukitoa watoto nusu yake wanahitaji huduma hii lakini watoaji wako 5,000 na vijiji tunavyo zaidi ya 14,000 utakuta vijiji zaidi ya 7,000 hawana wasaidizi,” amesema Olengurumwa.

Akizungumzia semina hiyo, Olengurumwa amesema wameiratibu ili kuunga mkono Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (Samia Legal Aid Campaign), inayoendelea nchi nzima.

“Tumeona mafunzo haya ni fursa kwa Watetezi lakini kuunga mkono kampeni ya Samia Legal Aid, sababu nyie wasaidizi wa kisheria ndiyo watekelezaji hivyo lazima tuwajengee uwezo kuhakikisha Taasisi za msaada zinakuwa zaidi,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema “hii ni dhana mpya sababu mwanzo tulikuwa na mafunzo ya  elimu kwa wanasheria, sisi tukaja na majaji na Sasa watoa msaada wa kisheria.

“Tunafanya hivi sababu elimu haina mwisho hata profesa anaendelea kuwa darasani kwa kuwa Kila wakati standard zinabadikika, sheria zinatungwa mpya na mazingira yanabadilika hivyo muendelezo wa elimu ni jambo la msingi itasaidia kuwa na Watetezi wenye uwezo wa kuwawezesha Watanzania kulinda haki za binadamu.

Naibu Mkuu wa Shule ya Sheria, Dk. Clement Mashamba, amesema wameanzisha kozi ya huduma ya msaada wa kisheria ili kuongeza umahiri kwa wanaoitoa.

“Mafunzo Maalum ya umahiri kwa wasaidizi wa Kisheria ni miongoni mwa malengo ya sheria yetu ya msaada wa Kisheria, kulikuwa na takwa lazima wapewe mafunzo na tumeanza na mafunzo ngazi ya chetu na baada ya muda tutaanza diploma mpaka tupate ithibati,” amesema Dk. Mashamba na kuongeza:

Wale wasaidizi ambao hawajapata masomo Maalum mnaweza kutumika fursa hiyo dirisha la usajili limeshafunguliwa. Haya ni mafunzo muhimu sababu yanamuandaa mwanafunzi kwenda kutoa huduma bora.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Msaada wa Kisheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Veronica Buchumi, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia wahusika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Dk. Mashamba amesema mafunzo haya ni ya muhimu sana, Sasa huduma za msaada tunazotoa kitu Cha msingi sana sababu wakati mwingine unaweza kusema tunawpaa msaada, lakini ubora ni kitu Cha msingi,” amesema Dk. Buchumi na kuongeza:

“Mafunzo haya yanalenga kuboresha huduma huduma tunazotoa Kwa Watanzania ambao hawaweI kukidhi gharama za mawakili.Wote wamekuja Kwa Nia ya kukuza ujuzi, kujifunza kanuni na tarativu zitakazosaidia kuboresha huduma ya msaada wa Kisheria.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!