Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya Hazina kuendelea kuwa juu kitaaluma
Elimu

Shule ya Hazina kuendelea kuwa juu kitaaluma

Spread the love

SHULE ya Msingi Hazina imeahidi kuendelea kuwa juu kitaaluma kwa kuhakikisha inakuwa na walimu mahiri na wenye wito wa kazi ya ualimu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma wakati a mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Alisema shule hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhimiza elimu bora kwa kuwalea wanafunzi kimaadili na kuwapa ushauri unaowawezesha kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

Wanafunzi wa shule ya msingi Hazina wakiingia kwenye mahafali yao yaliyofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

“Kwa kuzingatia kwamba dunia ya leo ni ya utandawazi ni jukumu letu kama walimu na walezi kuwaelimisha wanafunzi kuhusu kila wanachokifanya,” alisema

Alisema kwa miaka 17 tangu shule hiyo kuanzishwa imepata mafanikio makubwa kitaaluma kwani imekuwa na matokeo mazuri katika ngazi za wilaya, mkoa na hata kitaifa.

Alisema mwaka huu wameendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kuwa shule ya kwanza kiwilaya na katika mkoa wamefanikiwa kuingia kwenye kundi la kwanza la ufaulu (band 1) .

Wanafunzi wa shule ya msingi Hazina wakionyesha bunifu mbalimbali kwenye mahafali hayo

“Katika ngazi ya taifa wanafunzi wetu wote wamefanikiwa kufaulu huku shule yetu ikifanikiwa kupata daraja A la ufaulu katika mtihani wa taifa wa mwaka 2022 na kwa mwaka huu tunatarajia matokeo makubwa zaidi,” alisema

“Pia tumefanikiwa kuibua vipaji mbalimbali vya watoto kama mlivyoona kwenye maonyesho na hii ni dalili nzuri kwamba katika maisha yao ya baadae wataendelea vizuri sana,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!