Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwasse awaasa wajiolojia kuiishi ‘Vision 2030’ kupitia mkutano TGS
Habari Mchanganyiko

Dk. Mwasse awaasa wajiolojia kuiishi ‘Vision 2030’ kupitia mkutano TGS

Spread the love

Katibu Mkuu Wizara ya uvuvi na Uchumi wa buluu Dkt. Aboud Jumbe tarehe 11 Novemba 2023 ametembelea banda la STAMICO wakati wa  ufungaji wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS) uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wakati akiwa katika Banda la STAMICO Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar alipata maelezo ya  shughuli mbalimbali za Shirika kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO CPA (T) Dkt. Venance Mwasse.

Aidha  Dkt Mwasse alimwelezea Jinsi ya Shirika ilivyoingia Makubaliano (MoU) na Wizara ya Maji, Nishati na Madini  kuifikisha nishati ya mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema tahere 13 Novemba 2023 kutakuwa na kikao kazi cha Mashirikiano kati ya STAMICO, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar na taasisi zingine za Serikali na wadau kwa ajili ya kujadili njia bora ya kuifikisha nishati hii kwa Wananchi.

Naye Katibu Mkuu Dk. Aboud Jumbe  aliwashukuru STAMICO kwa ubunifu mkubwa wa uzalishaji wa nishati hiyo mbadala ya Rafiki briquettes inayozalishwa kutokana  na mabaki ya makaa ya mawe.

Pia ameitaka STAMICO kushirikiana pia na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu  katika kuhakikisha nishati hiyo inawafikia wavuvi na wakaushaji dagaa ambao wanatumia gharama ni kubwa kutumia mkaa unaotokana na miti kwa ajili ya kukaushia dagaa.

Amesema wafanyabiashara hao hutumia mkaa wa miti kwa wingi na kuchochea uharibifu wa mazingira.

Ameongeza kuwa kwenye kikao hicho cha tarehe 13 Novemba 2023 Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu inatakiwa kujumuika kwa dhati kama mmoja ya wadau wakubwa.

Awali akitoa salamu  kwa Washiriki wa Mkutano huo Dk. Mwasse aliwapongeza TGS kwa ubunifu wa kupeleka Mkutano mkuu Zanzibar.

Amesema hatua hiyo imeifanya STAMICO kupata manufaa mbalimbali ikiwamo nafasi ya kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Zanzibar.

Aidha, amewapongeza TGS kwa mada nzuri zinazozungumzia madini ya kimkakati ambayo kwa sasa dunia inahamia huko katika utafiti wa madini hayo.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Mwasse alizungumzia ‘Dira 2030’  inayoenda sambamba na kauli mbiu kuwa Madini ni Maisha na Utajiri na kusisitiza kuwa dhana hiyo inajikita katika kutafuta taarifa za kijiolojia.

Amesema taarifa za sehemu yalipo maji, petrol, mafuta ya aina mbalimbali ikiwamo madini na gesi, zitafahamika  na kusaidia nchi kwenye shughuli mbalimbali za uchimbaji.

Dk. Mwasse pia aliwaasa washiriki na viongozi wa TGS kuiishi  dira hiyo ambayo awali ilipata baraka kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na sasa STAMICO vilevile inaendelea kuiishi dira hiyo na kuhakikisha inafanikiwa.

Mkutano huu wa jiolojia Tanzania ambao umeambatana na maonesho umefungwa rasmi leo tarehe 11 Novemba 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa buluu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!