Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashungwa aahidi Tanzania Bara, Zanzibar kudumisha ushirikiano sekta ya ujenzi
Habari Mchanganyiko

Bashungwa aahidi Tanzania Bara, Zanzibar kudumisha ushirikiano sekta ya ujenzi

Spread the love

WAZIRI wa  Ujenzi, Innocent Bashungwa ameahidi kuendelea kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya ujenzi  ili uboreshaji wa miundombinu ya ujenzi upatikane katika maeneo yote ya bara na visiwani. Anaripoti Danson Kaijage, Mwanza (endelea).

Bashungwa ametoa kauli hiyo jana jijini Mwanza katika mkutano wa sita wa sekta hiyo uliobeba kauli mbiu ya “Ushirikiano imara kwa miundombinu na muungano imara”.

Pia ameahidi kusimamia kwa karibu mapendekezo na maazimio yote waliyokubaliana katika mikutano inayofanyika kwa faida ya pande zote mbili za muungano.

Aidha, Bashungwa amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu tangu aingie madarakani.

Amesema katika kipindi hicho kumekuwa na mageuzi makubwa kwenye sekta ya ujenzi ambayo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya utalii, elimu na afya na hivyo kukuza uchumi wa Taifa kiujumla.

Naye Mwenyekiti mwenza kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ), Dk. Khalid Mohamed amesema kwa kuzingatia kazi za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, sekta ya ujenzi imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema  miundombinu katika pande hizo mbili imeshamiri na hivyo kuchochea ukuaji wa utalii na hivyo kukuza uchumi wa taifa.

“Kwa kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa Rais Dk. Mwinyi tumepata mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za Mijini na Vijijini ambapo zaidi ya kilomita 846 za barabara zinaendelea kujengwa Unguja na Pemba kwenye mtandao wa barabara wenye takribani kilometa 1,344”, amesema Dkt. Mohamed.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

error: Content is protected !!