Saturday , 9 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi Hazina waonyesha vipaji vya hali ya juu.
Elimu

Wanafunzi Hazina waonyesha vipaji vya hali ya juu.

Spread the love

WANAFUNZI wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam wameonyesha vipaji vya aina yake walipokuwa kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wanafunzi hao walionyesha vipaji kama kuimba, kucheza, sarakasi na mitindo mbali mbali ya mavazi hali ambayo iliwafurahisha wazazi walioshuhudia mahafali hayo.

Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma alisema shule hiyo imekuwa na program ya michezo kwaajili ya kuangalia vipaji mbalimbali vya wanafunzi.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hazina wakionyesha vipaji vya

Alisema michezo mbali na kuimarisha afya za wanafunzi lakini inaweza kusaidia kwa wale wenye vipaji kuwa chanzo cha mapato kama baadhi ya wasanii waliofanikiwa.

Alisema Hazina itaendelea kuibua na kulea vipaji vya wanafunzi ili viweze kuwasaidia kwenye maisha yao ya kila siku kwani upo ushahidi wa watu waliofanikiwa kutokana na vipaji vyao.

“Kuna mwanafunzi mwingine anaweza kuwa wa kawaida darasani lakini akawa na kipaji kikubwa sana ambacho akikiendeleza anakuja kuwa msanii mkubwa sana na anaingiza fedha nyingi kwa hiyo utaratibu wa kuibua vipaji uwe endelevu kwa shule nyingi,” alisema Omari

Mmoja wa wazazi wa waliohudhuria mahafali hayo, Asha Aboubakary alipongeza shule hiyo kwa kuendesha program ya kuibua vipaji vya wanafunzi kwani wamejionea wenyewe namna wanafunzi walivyoonyesha umahiri kwenye sanaa.

“Kwa kweli tumeona wenyewe umahiri wa wanafunzi wa Hazina kwenye sanaa na mitindo mbalimbali kuanzia sarakasi, mitindo ya mavazi, kuimba na kucheza kwa hiyo vipaji huwa vinalelewa tumeona vipaji vingi ka hiyo wavilee vinaweza kuja kuwasiaida hawa watoto,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!