Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shibuda atumia samaki kuzungumzia utawala bora
Habari za Siasa

Shibuda atumia samaki kuzungumzia utawala bora

Spread the love

JOHN Shibuda, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama cha Ada- Tadea amesema, iwapo Watanzania watamchagua katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, atahakikisha wanaishi kwa furaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Shibuda alitoa ahadi hiyo jana jioni Jumanne tarehe 11 Agosti 2020 nje ya Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo Ndejegwa jijini Dodoma, baada ya Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage kumkabidhi fomu za kuteuliwa kugombea urais.

Mara baada ya kukabidhiwa akiwa mgombea wa 16 kuchukua fomu, Shibuda alisema “Naipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kila mmoja anayetaka kugombea kiti cha Rais anapewa fomu.”

“Pia, nampongeza Rais John Magufuli kwa kutoa tamko lake kuwa uchaguzi utakuwa wa amani, huru na haki kwani umewafanya wengi kujitokeza kwenye udiwani, ubunge na urais,” alisema Shibuda ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania

Kwa nyakati tofauti, Rais Magufuli amekuwa akisema, Serikali anayoiongoza, itahakilisha uchaguzi huo unakuwa wa amani, uhuru na haki huku akionya watakaojaribu kuuvuruga, watachukulia hatua kali za kisheria.

Katika ahadi zake Shibuda alisema, maana ya uongozi bora unaokidhi matakwa ya Watanzania, “maana yake ni kuonyesha njia, kiongozi bora maana yake hana mgogoro na afya yake, mgombea yeyote hususan kiti cha Rais anapaswa kuwa na afya njema ya uono wa akili, busara na hekima.”

Alisema, uongozi uko katika fumbo la samaki, “uozo wa samaki huanzia kichwani, uozo wa utawala bora huanzia kiti cha Rais, kwa hiyo ikiwa afya ya uongozi bora ina matata, mgogoro kwa kiongozi anayeongoza, basi taifa hilo huishia kwenye majanga.”

“Mimi ninawania nafasi hii kwa sababu kwani maana ya siasa ni rufaa, jicho kwa wananchi, serikali yangu itakuwa ni hisia kwa jamii, zitatanua wigo na maana ya demokrasia.

“Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa furaha na haki za binadamu zinasimamiwa na matumizi ya dola yanakuwa ni sahihi kwa maslahi ya jamii na taifa,” alisema Shibuda ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Ada-Tadea

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!