Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheikh Ponda mbaroni kwa kuandamana
Habari MchanganyikoTangulizi

Sheikh Ponda mbaroni kwa kuandamana

Spread the love

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini Tanzania, Sheikh Issa Ponda na wenzake  wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kosa kuandamana kwa lengo la kushinikiza kusimamishwa kwa mapambano ya Israel na wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza nchini Palestina. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Sheikh Ponda na wenzake wanaokadiriwa kufika tisa wamekamatwa leo Ijumaa Mnazi mmoja walipapanga kuanza maandamano  yao waliyolenga kufika mpaka Manzese Tip Top .

Maandamano hayo hayakufika popote baada ya kachero wa Jeshi  la Polisi aliyevaa kiraia alipoonekana kumzuia Sheikh Ponda na wenzake kufanya maandamano hayo.

Kachero huyo  alimtaka Sheikh Ponda aingie kwenye gari lao .

Kwa mujibu wa msaidizi wa Sheikh Ponda amesema kuwa kiongozi wao na wafuasi wengine tisa wapo kwenye mikono ya Polisi.

1 Comment

  • Kwani walivunja sheria gani? Lerngo lao lilikuwa ni sawa na la serikali. Katika Umoja wa Mataifa nchi yetu ilupiga kura ya kusimamisha mauaji ya Gaza. Na ndio lengo la Ponda. Sasa kosa liko wapi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!