Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) Deodatus Balile amesema kuwa ni muda muafaka wa kuwapa motisha wanafunzi katika tasnia ya habari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Balile ameyasema hayo leo Ijumaa katika Chuo kikuu cha Tumaini (Tudarco) baada ya kumkabidhi zawadi Mwanafunzi Patson Andungalile aliyefanya vizuri katika masomo ya uandishi wa habari chuoni hapo.
“Tumeshuhudia tasnia nyingine wafanyakazi, wanafunzi wanaofanya vizuri hupewa zawadi sasa ni wakati muafaka wa kuwatia moyo wanafunzi katika tasnia hii ili naye akimaliza ajue kuwa anatambulika” amesema Balile.
Balile amewataka wanafunzi wa taalama ya habari kuhakikisha wanajiandaa vizuri ili wakiingia kwenye vyombo vya habari wapate nafasi ya kuajiriwa.
Leave a comment