Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mahafali ya CBE yatia fora Dar
Elimu

Mahafali ya CBE yatia fora Dar

Spread the love

SERIKALI imevitaka vyuo vikuu kuwa na program atamizi na zile za uanagenzi ili kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuhangaika kutafuta ajira wanapomaliza. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, wakati wa mahafali ya 58 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNICC.

Kwenye mahafali hayo kulikuwa na wahitimu 1,226 wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili (Masters Degree).

Alisema utandawazi umesababisha mabadiliko makubwa kwa kasi yanayogusa kila nyanja ya maisha hivyo ni muhimu kutafuta njia ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwenye maisha.

Alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua umuhimu wa elimu ya ujasiriamali waliyoipata chuoni hapo kwani itawafundisha namna ya kuwa wabunifu na kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdalah, akimtunuku mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakati a mahafali ya 58 ya chuo hicho ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

“Kwa elimu mliyoipata mnatakiwa kwenda kutengeneza ajira kwa wengine badala ya kuwa tegemezi wa kuhangaika kutafuta kuajiriwa nyinyi nendeni mkajiajiri na kuajiri wengine,” alisema Dk. Hashil

“Nyinyi mmepata elimu bora kwa hiyo nendeni mkaitumie kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayosaidia ustawi wa jamii na chuo kimeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mnapotoka CBE mnakuwa na uwezo wa kujiajiri,” alisema

Aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa maono mazuri yaliyisababisha kuanzisha program atamizi ya baishara ambayo inawapa wanafunzi uwezo wa kujifunza usimamizi a biashara kwa vitendo wanapokuwa shule.

Alisema program hiyo na ile ya uanagenzi inawawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakiwa shule hivyo wanapomaliza masomo hawasumbuki kutafuta ajira.

Dk Hashil pia aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuanzisha masomo ya Shahada ya Uzamili katika usimamizi wa biashara (MBA), mtandaoni kwani inaonyesha ujasiri na uthubutu wa CBE katika kutoa elimu bora na inayokidhi mahitaji ya sasa ya dunia.

Kaimu Mkuu a Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa chuo hicho kwenye mahafali ya 58 ya chuo hicho yaliyofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dk. Hashil Abdalah.

“Kuzindua program hizi kunaweka iwango vipya vya ubora   na upatikanaji wa elimu ya juu nawapongea kwa kufungua milango ya fursa kwa wanafunzi na wataalamu ambao wanatafuta kujiendeleza bila kujali umbali,” alisema

Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini na kupongeza mafanikio ya chuo cha CBE na itaendelea kufanyia kazi changamoto ya miundombinu ya vyuo vyote vya elimu ya juu kikiwemo chuo hicho ili kuvuka changamoto hizo.

Alikitaka chuo hicho kuwaendeleza walimu wake na kuwekeza kwenye program za kisasa za kufundisha, mbinu za kujifunza na mitaala ili kuhakikisha elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

“Wekezeni kwenye vifaa vya teknolojia madarasani ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia na chuo kifanye tafiti zinazolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kutoa rasilimali kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika miradi ya utafiti na uvumbuzi,” alisema

Meza kuu kwenye mahafali Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), wakati a mahafali ya 58 ya chuo hicho ambayo yamefanyika Ijumaa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Naye Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, alisema wahitimu hao wamehitimu katika masomo mbalimbali yakiwemo ya usimamizi wa biashara, masoko, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na ugavi.

Profesa Lwoga alisema chuo hicho kimejitahidi kwa kiwango kikubwa kuwafundisha wahitimu ili wanapohitimu waweze kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kuhangaika kutafuta ajira.

“Tangu mwaka 2022 tulianzisha program atamizi za biashara ambapo wanafunzi wetu wenye mawazo ya biashara na bunifu mbalimbali wanatuletea mawazo yao tunayalea na wanaweza kuanza kufanyabiashara wakiwa chuoni na tunashirikiana na taasisi mbalimbali,” alisema

“Kuna wanafunzi wa CBE wameanza kujiajiri wakiendelea na masomo na kwa sasa wamehitimu tunatarajia waendeleze biashara zao na wakaajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!