Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sheikh Ponda awataka wanawake waislamu washiriki masuala ya kitaifa
Habari Mchanganyiko

Sheikh Ponda awataka wanawake waislamu washiriki masuala ya kitaifa

Spread the love

KATIBU wa Shura ya Maimsmu, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewataka wanawake wa kiislamu washiriki katika masuala ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa Maendeleo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Sheikh Ponda ametoa wito huo leo tarehe 16 Septemba 2023, katika Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania, lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Nawashauru mshirki katika masuala ya Maendeleo ya nchi, tumeelezwa rekodi zetu hazionyeshi kama tunashiriki mambo yanayotuhusu nchi wanawake wa kiislamu hawaonekani kushiriki mambo ya nchi. Sababu mambo ya nchi yanaguda kwa namna moja au mbalimbali na kutoshriki maana yake unatoa nafasi watu washiriki Kwa niaba yako,” amesema Sheikh Ponda.

Kiongozi huyo wa dini amesema kuwa, kutokuwepo ushiriki wao wa kutosha katika masuala ya kitaifa ikiwemo vikao vya maamuzi, kunasababisha maslahi yao kutolindwa.

Aidha, Sheikh Ponda amesema kushiriki katika masuala ya uongozi sio dhambi.

“Tunaposhiriki masuala ya nchi unajitetea mwenyewe na usiposhiriki unamuachia mwingine kwenye nafasi ile ya maamuzi. Tunapofanya mikutano ya kitaifa mnatakuwa mshiriki,” amesema Sheikh Ponda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!