Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa malezi, makuzi ya mtoto wapigwa msasa
Habari Mchanganyiko

Wadau wa malezi, makuzi ya mtoto wapigwa msasa

Spread the love

WADAU wanaoshughulika na malezi na makuzi ya watoto wametakiwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya Programu Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT -MMMAM) ili kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto wa mkoa wa Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu wakati wa ufunguzi kikao cha wadau hao kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kilichofanyika juzi tarehe 16 Septemba 2023 yaliyofanyika mkoani humo.
Kikao hicho kililenga kujadili afua mbalimbali za namna ya kuboresha malezi na makuzi ya watoto.

Baadhi ya washiriki wa kikao hicho.

“Mradi huu unagusa maeneo tofauti tofauti ikiwemo lishe ya mtoto, malezi kuanzia ujauzito hadi miaka minane na fursa za ujifunzaji wa malezi ya awali ya mtoto,” amesema Gugu.
Amesema Dodoma ina takribani wadau 410 wanaoshirikiana na Serikali katika kufanikisha program hiyo ambayo ni muhimu hasa ikizingatiwa mkoa wa Dodoma unakabiliwa pia na lishe duni kwa watoto.

Aidha, amewaasa akina mama na walezi kuzingatia nafundisho ya lishe yanayotolewa na wataalamu kuanzia kipindi cha ujauzito hadi malezi ya Mtoto.

“Kwa kipindi cha 2022/2023 jumla ya kina mama / walezi 191, 662 kati ya 200, 981 walio na watoto wenye umri wa miezi 0 – 23 walipewa unasihi juu ya kuwalisha watoto uliofanywa na watoa huduma ya afya sawa na asilimia 104.60. Hii ninaonyesha ni kwa namna gani unapomlinda mtoto kwa kumpa lishe bora, itasaidia katika makuzi yake” ameongeza, Gugu.

Naye Mratibu wa Malezi na makuzi ya watoto Stella Matemu amesema lengo kuu la kikao hicho ni kuwatambua wadau pamoja na kujadili afua mbalimbali zinazopatikana kwenye mradi huu ulioazinduliwa rasmi mwaka 2021 kitaifa.

Amesema kwa mkoa wa Dodoma mradi huo ulizinduliwa Septemba 2022 ukihusisha maeneo matano ambayo yanahusiana na malezi na makuzi ya mtoto kuanzia miaka 0 – 8 nayo ni elimu, afya, lishe, malezi na mwitikio,” amesema Matemu.

Hata hivyo, mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Watoto na Makundi maalumu, Joel Mwakapala amesema kuwa asilimia 90 ya ubongo wa mtoto unakua akiwa katika umri wa miaka 0 hadi 8 huku akielezea namna program hii inavyoleta matokeo chanya kwa jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Vitalu 19 vya madini vyazalisha ajira 12,000 Songwe

Spread the loveZAIDI ya vijana 12,000 kutoka Wilaya ya Songwe mkoani Songwe...

Habari Mchanganyiko

Mmoja auawa kwa tuhuma za kuiba sokoni, Polisi walaani

Spread the loveMwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina lake  ameuawa  na wananchi wenye...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

error: Content is protected !!