Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali Yapongeza Jitihada Za Shirika la Bima Zanzibar Kuboresha Upatikanaji Huduma
Habari Mchanganyiko

Serikali Yapongeza Jitihada Za Shirika la Bima Zanzibar Kuboresha Upatikanaji Huduma

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akili amepongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kuendelea kubuni namna mbalimbali katika kurahisisha upatikanaji wa huduma ya bima kwa wateja wake na jamii kwa ujumla,  hatua aliyoitaja kuwa inakwenda sambamba na nia ya serikali katika kuboresha sekta ya Bima nchini kwa kupanua ushiriki wa wananchi katika shughuli za kibima. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa huduma ya kidijitali ya VodaBima kupitia ushirikiano wa kiutendaji baina ya Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) na Kampuni ya Vodacom Tanzania iliyofanyika visiwani Zanzibar jana tarehe 3 Novemba, 2021 Dk. Akili alisema hatua hiyo inadhihirisha nia ya Shirika hilo ya kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi na kuwapatia huduma ya bima karibu zaidi na maeneo yao kulingana na azma ya serikali.

“Kupitia huduma hii ya Vodabima wananachi sasa watapata huduma za kibima kwa ukaribu zaidi kupitia simu zao za mkononi na hivyo kuongeza urahisi katika upatikanaji wa huduma hiyo na  kuongeza wigo wa kuwafikia wateja na wanachi kwa ujumla na hivyo kukuza sekta ya bima nchini.”

“Na hii ndio sababu nawapongeza sana ZIC kwa juhudi zao za kuendelea kuwafikia wanachi na wateja wao kwa ukaribu na huu ukiwa ni muendelezo  wa jitihada walizozifanya hivi karibuni kwa kuingia kwenye makubaliano ya kiuendaji kama haya na Shirika la Posta Tanzania. Nadiriki kusema hii ni heshima na moja ya mafanikio kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoadhimisha mwaka mmoja tangu Rais Dk. Hussen Ali Mwinyi aingie madarakani.’’ Alisema.

Zaidi, Dk. Akili aliipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ushirikiano huo huku akiiomba kampuni hiyo kuendelea kujitanua zaidi katika visiwa hivyo ili wananchi waendelee kufaidi zaidi huduma za shirika hilo zikiwemo zile za kibiashara na kijamii kupitia simu za mkononi.

Kwa upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dk. Mussa Juma pamoja na kupongeza taasisi hizo mbili kwa ushirikiano huo kupitia ubunifu, alitoa wito kwa makampuni ya bima nchini kuendelea kubuni zaidi huduma mbalimbali za kibima ili kuongeza wigo wa huduma za kibima sambambana na njia (distribution channels) za kuwafikia wateja wao.

“Hiki nachokishuhudia hii leo ni mwanzo mzuri kwasababu tulianza ushirikiano na mabenki kupitia huduma za bancassurance na sasa tunaingia kwenye kampuni za simu na Vodacom wanakuwa wa kwanza kufanikisha hili nawapongeza sana! Pongezi pia kwa ZIC kwa kuchangamkia fursa hii naomba na wengine waendelee kuiga na kubuni namna zaidi ya kuwafikia wananchi kwasababu bado tupo nyuma katika ufikiaji wa huduma za kibima kwa wananchi,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima Zanzibar(ZIC),  Arafat Haji alisema mbali na kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya Bima hapa nchini, hatua hiyo ni mwendelezo wa mkakati wa Shirika hilo katika kusaidia jamii kufikiwa na huduma za bima kwa ukaribu zaidi  na kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma hiyo na kukuza sekta ya bima nchini kwa ujumla.

“Mkakati huu unakuja tukitambua fika kwamba kwasasa ufikiwaji wa huduma ya bima kwa wananchi ni asilimia 30 tu hivyo jitihada zaidi zinahitajika. Tunaamini kupitia huduma hii ya VodaBima inayotumia miundombinu bora ya teknolojia ya M-Pesa na mtandao mpana wa Vodacom ambayo inapatikana katika maduka ya Vodacom nchini kote tunakwenda kuwafikia wateja wetu kwa urahisi zaidi huku pia tukiwahakikishia usalama zaidi katika utoaji wa huduma  zetu za kibima…tunaomba sana watuunge mkono!’’ alisema.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Biashara M-Pesa, Rashid Tulisindo alisema kupitia huduma hiyo ya VodaBima kampuni hiyo inakusudia kuziba pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za Bima.

Alisema VodaBima inatumia miundombinu bora ya teknolojia ya M-Pesa na mtandao mpana wa Vodacom ambayo inapatikana katika maduka Vodacom nchini kote kuhakikisha usalama, urahisi wa upatikanaji wa huduma za bima.

“VodaBima ni huduma ya kwanza ya aina yake sokoni, kupitia huduma hii tunakwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima za Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) pamoja na mfumo wa kufanya madai. Kwa sasa tunatoa bima ya vyombo vya moto ikiwemo magari na pikipiki lakini tunapanga kuleta bidhaa zingine ili kukidhi mahitaji ya wateja na kwenda sambamba na mabadiliko ya soko,” alisema Tulisindo.

Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Bima Tanzania(TIRA) Bi. Khadija Issa Said, baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wafanyakazi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) na wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!