Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yapanga kukusanya Sh trilioni 47
Habari za Siasa

Serikali yapanga kukusanya Sh trilioni 47

Spread the love

WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amewasilisha  mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya 2024/25, bungeni jijini Dodoma, akisema Serikali imepanga kukusanya na kutumia Sh. 47.42 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Mwigulu amewasilisha mwongozo huo leo tarehe 6 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, akisema makadirio hayo yamezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo mwenendo halisi wa ukusanyaji mapato, viashiria vya uchumi jumla na jitihada zinazochukuliwa na Serikali kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato.

“Katika mwaka 2024/25, Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Sh bilioni 47,424.9 (Sh. 47.42 trilioni). Makadirio ya mapato yamezingatia vigezo mbalimbali. Aidha, kwa upande wa matumizi, makadirio yamezingatia mahitaji halisi ya ugharamiaji wa deni la Serikali, mishahara ya watumishi pamoja na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati inayoendelea,” amesema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo wa fedha amesema mapato ya ndani ikijumuishwa ya mamlaka za serikali za mitaa, yanakadiriwa kuwa Sh. 34.43 trilioni, ambapo mchango wake katika bajeti unatarajiwa kuwa asilimia 72.6.

Dk. Mwigulu ametaja vipaumbele vya bajeti hiyo, ikiwemo uendelezaji na utekelezaji miradi ya kilelezo, hususan mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere, kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (SGR), ujenzi bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanzania.

Vipaumbele vingine ni, uimarishwaji wa uwezo wa uzalishaji viwandani, ukuzaji biashara na uwekezaji na kuchochea maendeleo ya watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!