Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia kukata mzizi wa fitna tozo miamala ya simu
Habari za Siasa

Samia kukata mzizi wa fitna tozo miamala ya simu

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema majibu ya kilio cha wananchi juu ya tozo ya miamala ya simu, yatapatikana tarehe 29 Julai 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, akiwaapisha mabalozi 13 aliowateua tarehe 22 Mei 2021.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amesema majibu hayo yatapatikana baada ya kamati iliyoundwa na Serikali, kupitia maoni ya wananchi kuhusu tozo hiyo, itakapowasilisha mapendekezo yake.

“Hili la miala ya simu, kutuma na kupokea fedha ambapo tulianza huu mfumo Julai, lakini baada ya kuanza kelele nyingi zikatokea. Wananchi wakalalamika nasi kwa sababu ni Serikali sikivu tukapokea maoni yao, tulipokea kama wiki,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameongeza “tunatarajia kupokea maoni ya kamati tuliyounda tarehe 29 Julai 2021, yaani kesho kutwa na baada ya hapo tutaujulisha umma tunakwendaje katika hili.”

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia amesema, Serikali haitaiondoa tozo hiyo, bali itaangalia njia nzuri ya kuitumia pasina kuathiri wananchi.

“Hizi tozo nataka niseme zipo, ila tutaangalia njia nzuri ambayo haitaumiza watu. Serikali ipate na wananchi wapate kazi iendelee,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema, Serikali yake iliamua kuweka tozo hiyo ili ipate fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, itakayosaidia kutatua changamoto za wananchi ikiwemo, uhaba wa maji na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Tozo hizo zinazotozwa katika miamala ya simu, zilianza kutumika kuanzia tarehe 15 Julai mwaka huu.

Ambapo Serikali inatoza kuanzia Sh. 10 hadi 10,000, katika muamala wa kutuma au kutoa pesa, kulingana na thamani ya muamala wa fedha husika.

Kupitia tozo hiyo, Serikali inatarajia kukusanya zaidi ya Sh. 600 bilioni, katika mwaka wa fedha wa 2021/22, ambazo zitatumika katika kuimarisha huduma za afya, miundombinu ya barabara na elimu.

Kwa mujibu wa Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, fedha zitakazopatikana kupitia tozo hiyo, zitajenga vyumba vya madarasa 10,806, vya shule za msingi na sekondari.

Pia, zitajenga shule za sekondari za kata 300 na shule za sekondari za sayansi za wasichana 10. Kwenye afya, fedha hizo zitajenga na kukamilisha zahanati 756 zahanati.

Kwenye miundombinu, fedha hizo zitajenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 250, kupandisha hadhi barabara za udongo kuwa changarawe, urefu wa kilomita 5,834 na madaraja makubwa 64.

1 Comment

  • TUPO NA MADINI YAKUTOSHA TZ NA KAMA HAYATOSHI TUAZISHE KILIMO CHA BANGE ILI TUWEZE KUUZA NJE YA NCHI,TUNAWENZA KULIMA NA KUUZA BAGE ICHI ZA EUROPA KWA MATILION YA DOLLER KWA MWAKA KAMA WENZETU WA UGANDA. VYANZO VYA PESA VIPO ILA MNAPENDA KUTUUMIZA SISI RAIYA WA HALI YA CHINI MALOFA HUU NI UZAIFU WA MILEMBE BUNGE NA SERIKALI.TUNAPENDEKENZA TOZO YA MIAMALA IWE ILE ILE ILIVYOKUWA KABLA YA KUPANDISHWA ILI MZUNGUMKO WA PESA KWA RAIA MASKINI UWENDE KWA MWENDO WA SPEED ILE ILE TULIYOIZOEA NA SIVINGENEVYO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!