June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Mabalozi msikae kimya Tanzania ikichafuliwa

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka mabalozi wasikae kimya taswira ya Tanzania inapochafuliwa kimataifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, akiwaapisha mabalozi 13 aliowateua tarehe 22 Mei mwaka huu.

“Ni jukumu lenu kuhakikisha mnalinda taswira yetu kwenye anga la kimataifa, kwa kuisemea nchi yetu vizuri na pale kwenye upotoshaji, jukumu lenu kunyoosha taarifa na kutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu maamuzi mbalimbli tunayochukua,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameongeza “ hampaswi kuwa kimya, nitashangaa balozi unaulizwa taarifa ya nyumbani katika nchi uliopo, unasema sijapata taarifa kwa hiyo sijui kinachoendelea. Huo sio ubalozi, balozi lazima awe na taarifa.”

Wakati huo huo, Rais Samia amewaagiza mabalozi kujiepusha na vitendo vinavyohujumu nchi.

“Jukumu lenu kuhakikisha mnalinda maslahi ya nchi yetu popote kule mtakapo kuwepo. Kama mnavyojua dunia inaedeshwa kwa ushindani miongoni mwa mataifa. Kutokana na ushindani huo wakati mwingine kumekuwa na hujuma zenye lengo la kuhujumu usalama na shughuli za kiuchumi katika nchi,” amesema Rais Samia.

Mabalozi walioapishwa, ni Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo, aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania, Nchini Rwanda. Robert Kainunula Kahendaguza (Balozi Vienna, Austria) na Edwin Novath Rutegaruka (Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi).

Wengine ni, Caroline Kitana Chipeta (Balozi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria). Agness R. Kayola (Balozi na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda) na Masoud A. Balozi (Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar).

Caesar George Waitara ( Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia).
Swahiba Habibu Mndeme (Balozi na Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika). Maulidah Bwaakheir Hassan (Balozi Ofisi ya Rais Ikulu).

Alex Gabriel Kallua ( Balozi Ofisi ya Rais Ikulu). Said Juma Mshana (Balozi Ofisi ya Rais Ikulu). Fredrick Ibrahim Kibuta (Balozi Ofisi ya Rais Ikulu) na Hoyce Anderson Temu (Balozi na Naibu Mkuu wa Kituo cha Geneva).

error: Content is protected !!